Polisi nchini Uganda wamemkamata muuguzi kwa tuhuma za kubaka na jaribio la kuwabaka wagonjwa wawili wajawazito katika Hospitali ya Entebbe Grade B.
Muuguzi huyo aliye mafunzo alikamatwa Jumamosi, Februari 18, jioni na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Entebbe Central.
Naibu Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala, Luke Owoyesigire alisema mshukiwa, Kutesa Denis, alikuwa akiwatambua waathiriwa wake kutoka wodi ya Wanawake.
Kisha aliwawekea dawa ya kuwapoteza fahamu inayoshukiwa kuwa chloroform kabla ya kuwanyanyasa kingono.
"Dawa inayoshukiwa kuwa ya chloroform ilipatikana kutoka kwa makazi yake katika hospitali hiyo, na barua ikapatikana ambapo aliomba kuombewa dhidi ya mawazo machafu aliyokuwa nayo," Owoyesigyire alisema kwenye taarifa, akiwataka waathiriwa wengine kujitokeza, akisema kwamba inawezekana mtuhumiwa aliwanyanyasa wanawake wengine.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Peterson Kyebambe alisema kuwa tukio hilo sasa limewachochea kuongeza tahadhari na na kuimarisha usalama kwa kufunga kamera zaidi za CCTV.
Via: Tuko News