ASKARI WA JWTZ ALIYETAKA KUMGONGA TRAFIKI AFIKISHWA MAHAKAMANI


Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ ), MT 89487 CPL Hamis Ramadhan (36) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kukataa amri halali.


Mshitakiwa huyo amesomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Vailet Kyendesya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rahim Mushi, Vailet amedai Februari 07,2023 Mshtakiwa akiwa eneo la Mlimani City Barabara ya Survey, Kinondoni, Dar es Salaam akiendesha gari namba T. 433 ALB Nissan Patrol alisimamishwa eneo la kivuko cha watembea kwa miguu na Askari Polisi ambapo alikaidi na kuanza kumsukuma Askari kwa gari yake.


Kyendesya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa, baada ya kusomewa shtaka hilo Mshtakiwa alikana makosa yake na kuachiwa kwa dhamana, ambapo kesi imehairishwa hadi March 6, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.


Itakumbukwa Feb 10,2023 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumchukulia hatua Dereva wa gari aina ya Nissan Patrol aliyeonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni akikaidi amri ya kusimama iliyotolewa na Askari wa usalama barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم