Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC AAHIDI KASI NA UFANISI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU MAPYA





Mkurugenzi Mtendaji wa TIC akiwasili makao makuu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuteuliwa kuongoza Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambapo amepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dkt. Binilinth Mahenge pamoja na Menejimenti leo Februari 06, 2023 Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na uongozi Dkt. Mahenge amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara na kufanya kwa vitendo kujenga imani kwa wawekezaji kuwa Tanzania ni mahala salama kwa uwekezaji.


Dkt. Mahenge amemshukuru Rais Samia na kusema kuwa sasa mhimili wa bodi ya TIC umekamilika kwa uteuzi wa Katibu wa Bodi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji.


Mkurugenzi Mtendaji amemshukuru Mhe. Rais kwa kumteua kuongoza Kituo cha Uwekezaji na ameishukuru Bodi pamoja na Menejimenti ya TIC kwa ukaribisho na kusisitiza kuwa TIC ina sehemu kubwa ya maono makubwa ya Mhe. Rais na kwamba amekuja kuongeza nguvu.


“Nimekuja kuongeza nguvu kwenye utendaji wa majukumu ya Kituo na ubunifu kwenye mambo mapya na ushauri kwa serikali kuhusiana na maswala mazima ya kuvutia na kukuza Uwekezaji Tanzania”, amesema Teri.


#tunarahisishauwekezaji

#wekezatanzania

#kaziiendelee

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com