Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA, MFUMUKO BEI YA CHAKULA WALETA MJADALA, MDIMI AAPISHWA



Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makunde (kulia) akimpatia miongozo ya Baraza diwani mpya wa Mwamalili James Mdimi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamewasilisha taarifa za maendeleo ya kwenye Kata zao, pamoja na kubainisha changamoto ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi wa Manispaa hiyo.

Madiwani wamewasilisha taarifa zao leo Ferbruari 9, 2023 kwenye kikao cha Baraza cha kawaida cha robo tatu ya mwaka, ambacho kilienda sambamba na Uapisho wa Diwani mpya wa Mwamalili James Mdimi, ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa diwani wa Kata hiyo Paul Machela aliyefariki dunia.

Madiwani wakiwasilisha taarifa zao kila mmoja alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, huku wakibainisha badhi ya changamoto ambazo zinahitaji kutatuliwa ikiwamo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, upungufu wa matundu ya choo, upungufu wa walimu, watendaji, ukamilishaji maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Changamoto zingine zilizowasilishwa ni kasi ndogo ya usambazaji wa Nishati ya umeme hasa Kata ya Mwamalili, pamoja mfumuko wa bei ya vyakula, na kuiomba Serikali iendelee kutoa msaada wa chakula cha bei nafuu ili kuwanusuru wananchi na baa la njaa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akitoa majibu kwenye baraza hilo, amesema changamoto zote ambazo zimewasilishwa watazifanyia kazi, pamoja na zingine tayari zipo kwenye utekelezaji.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Andrew akiwasilisha taarifa za Kata yake kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Diwani wa Ndala Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akiwasilisha taarifa ya Kata yake kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Diwani wa Masekelo Peter Koliba akiwasilisha taarifa ya Kata yake kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe (kulia) akiwa na Katibu wa CCM wilaya hiyo Ally Majeshi, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

James Mdimi akiapa kuwa Diwani wa Mwamalili, (kulia) ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro.

Diwani mpya wa Mwamalili James Mdini akiapa kiapo cha maadili, (kulia) ni Gerald Mwaitebele Katibu msaidizi Ofisi ya Rais Secretarieti ya maadili viongozi wa umma Kanda ya Magharibi.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Anold Makombe (kushoto) akimpatia Nasaha diwani mpya wa Mwamalili James Mdimi mara baada ya kumaliza kula Kiapo cha kuwa Diwani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com