Majina ya watu 14 wa familia moja waliofariki katika ajali iliyotokea jana Ijumaa usiku wilayani Korogwe mkoani Tanga,Tanzania yametajwa.
Ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Korogwe imesababisha vifo vya watu 17 wakiwemo ndugu hao wa familia moja na kujeruhi 12.
Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Salma Sued na kunukuliwa na Mwananchi Digital imetaja ndugu waliofariki ni Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema na Godwin Mrema.
Wengine ni Yusuph Saimon, Zawadi Mrema, Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina A Lamosa, Evelina Cosmas Mrema na watoto wawili (mtoto wa binamu na mtoto wa Julieth).
Rais Samia Suluhu ameeleza kusikitishwa na ajali ya gari iliyosababisha vifo vya watu 17 mkoani Tanga.
Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar es Salaam kwenda Moshi kwenye mazishi.
Social Plugin