Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kulia,kushoto ni Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi wilayani Kishapu Ezibon Mathias.
Na Sumai Salum, KISHAPU
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo amemshauri Mkuu mpya wa Polisi wilaya hiyo (OCD) Ezibon Mathias kufanya kazi kwa ufanisi na weledi.
Ameyasema hayo leo 15.2.2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya halmashauri hiyo baada ya hivi Karibuni kupandishwa cheo kutoka Mkuu wa upelelezi wilaya hiyo hadi kuwa Mkuu wa Polisi wilaya.
"Wakati ukiwa Mkuu wa upelelezi ulikuwa unafanya sana kazi na pia wakati OCD aliyekuwepo akiondoka unapokaimu nafasi yake ulikuwa unatosha kile kiti, ndio maana umepandishwa cheo tunatambua pia utendaji kazi wako na tunatamani kutosikia tatizo la ubambikiaji kesi na mnatakiwa kuwa wepesi kufika eneo la tukio na uwaambie wasidizi wako kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wananchi na sio kuwaumiza" amesema Butondo.
Aidha Butondo amemtaka Mkuu huyo wa Polisi kuimarisha mahusiano katika kuboresha ulinzi wa wananchi na mali zao ndani ya jamii licha ya kukabiliwa na changamoto za uhaba wa magari.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya ameamuahidi Mkuu huyo wa Polisi kumpatia ushirikiano ili kuhakikisha amani inaendelea kutawala wilayani humo.

Social Plugin