Fainali ya ligi ya miaka 46 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikihusisha timu 8 wilayani Kishapu mkoani Shinyanga imemalizika kwa Kishapu Veteran kuibuka kidedea kwa kwa kuichapa Kishapu Sekondari bao 1- 0.
Ligi hiyo iliyoanza tarehe 23/1/2023 ikiwa na jumla ya timu nane na imemalizika 31/1/2023 katika viwanja vya shule ya msingi mhunze Wilayani Kishapu mkoani ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude ambaye ametoa pongezi kwa timu zote zilizoshiriki mashindano hayo ya kirafiki kutoka Kata ya Kishapu.
"Mbali na pongezi zangu kwa timu zote nimpongeze pia Diwani wa Kata hii ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson ambaye amekuwa kiongozi mwenye upekee kwa kuanzisha mashindano haya ambayo yan alengo hasa la kukuza vipaji vya vijana wetu hasa vijana wa Sekondari ambao waliingia fainali na kuwa washindi wa pili na ningependa mashindano haya yanapoisha hii Leo asiishie hapo aendelee kwa sababu hili ni jambo zuri na la kuigwa", amesema Mkude.
Aidha Mkude ametoa zawadi ya masufuria makubwa ya kupikia yenye thamani ya Tsh.180,000 kwa Diwani wa Kishapu kwa lengo la kusaidia shughuli za chama huku akikabidhi zawadi zilizoandaliwa na kamati ya maandalizi ya ligi hiyo, vyeti kwa timu shiriki zote huku mshindi wa kwanza na pili wakipewa vyeti na pesa.
Hata hivyo mwandaaji wa ligi hiyo na Diwani wa Kata ya Kishapu Bw. Joel Ndettoson amewapongeza washiriki wote na kuwataka washindi wa pili na wa tatu kutokata tamaa kwani wanayo nafasi nyingine ya kushinda ambapo amesema lengo hasa la yeye kuanzisha ligi ni kuadhimisha miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi na kuwaweka wananchi na vijana wote wa Kishapu pamoja kwa lengo la ustawi wa maendeleo ya Kata.
"Kipekee nimshukuru mgeni rasmi na watu wote mliojitokeza kwa ajili ya siku hii na siku zilizopita za michezo ya timu zote 8 zilizokuwa na utayari wa kushiriki jambo hili wanafunzi wameonesha uwezo mkubwa katika mchezo kwa kufika fainali kiukweli mmejitahidi na nipende kuwaahidi kuwa mnamo mwezi Machi tutaanza tena ligi nyingine hivyo timu zote shiriki za sasa na zingine tuwe na utayari kwa hilo".amesema Ndettoson.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bw. Colonely Lugoda kwa niaba ya kamati amemtunuku cheti cha Pongezi mgeni rasmi katika hafla hiyo kwa utayari aliouonesha tangu uzinduzi wa ligi ukiambatana na upandaji miti katika kijiji cha Kishapu hadi kufikia fainali.
Sambamba na hayo ligi hiyo ilikuwa na jumla ya timu 8 ikiwemo Kishapu Veteran fc,Kishapu Sekondari,Homeboys fc (Sulagi),Mwabusiga fc, Isoso fc,Majimaji fc pamoja na Matale fc huku Salum Mbwene (veteran) akiibuka mdakaji Bora,Mwandu Jilala (Kishapu Sekondari) mchezaji Bora Musa juma (talentfc) mfungaji bora na mshindi wa tatu wa ligi akiwa ni Talent fc.
Katika mchezo huo, Kishapu veteran I waliongoza kwa mabao mawili la kwanza likifungwa na Richard Mwashambwa dakika ya 34 lapili likifungwa na Minza Jonh dakika ya 43 na baadae kipindi Cha pili mchezo ukianza na kumalizika kwa kasi Kishapu Sekondari walijipatia mabao mawili kutoka kwa Methew dakika ya 80 na la pili dakika ya 90 kiasi ya kupelekea waingie penati ambayo Amani Abeid akaipaisha Veteran kwa bao moja' kwa sufuri.
Social Plugin