Mwanaume mmoja kutokea nchini Ujerumani ambaye aligunduliwa kuwa na virusi vya UKIMWI ametangazwa kuwa amepona na hana tena virusi hivyo baada ya kupokea chembechembe za seli shina zilizostahimili virusi hivyo kupitia upandikizaji wa uboho (uroto) uliokusudiwa kutibu saratani ya damu (Leukemia).
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Nature Medicine mapema wiki hii umesema Mtu huyo alikuwa anafuatiliwa kwa zaidi ya miaka tisa baada ya upandikizaji uliofanyika mwaka 2013 na sasa kuna ushahidi mkubwa kwamba amepona, kitendo hicho kimefanikiwa baada ya Timu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Düsseldorf nchini Ujerumani kuua seli za saratani za Mgonjwa na kuweka seli ambazo hazina CCR5 kipokezi ambacho chembe za VVU hutumia kuambukiza seli nyingine mwilini.
Mnamo mwaka 2018, Mgonjwa huyo aliacha kupokea matibabu ya kurefusha maisha (ART), tiba ambayo huviweka virusi hivyo katika viwango vinavyoweza kudhibitiwa na amebaki bila VVU tangu wakati huo, taarifa hiyo imesema, yeye ni mmoja wa Watu wachache waliopata matibabu hayo kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na Timothy Ray Brown ambaye alipandikizwa uboho ambao pia uliondoa saratani ya damu (Leukemia) huko jijini Berlin mnamo 2007 na Adam Castillejo, ambaye alitangazwa kuwa hana maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) jijini London 2019.
Ingawa njia hii ya tiba haina uwezekano wa kutumiwa na Wagonjwa wasio na saratani kwa sababu ya viwango vyake vya hatari, utafiti unatoa uthibitisho zaidi kwamba VVU inatibika na sio kama ilivyofikiriwa hapo awali pia inatoa matumaini kwa siku za karibuni kuwa kuna uwezekano wa utafiti mwingine kufanyika ili kutafuta tiba ya UKIMWI “Utafiti unaonesha kuondoa virusi
Social Plugin