MILIONI 15 ZA TUZO USHINDI WA USAFI WA MAZINGIRA MANISPAA YA SHINYANGA ZATUMIKA KUNUNUA PIKIPIKI ZA MAOFISA AFYA MAZINGIRA

Maofisa Afya Mazingira Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Pikipiki ambazo wamepewa kwa ajili ya kusimamia hali ya usafi wa mazingira na kuufanya mji wa Shinyanga uendelee kuwa msafi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga mwaka jana iliibuka mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya kundi la Manispaa ya Shinyanga na kupewa zawadi ya fedha Sh. Milioni 15.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza leo Februari 10, 2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, amesema fedha ambazo walizipata  kwenye ushindi wa Tuzo ya usafi wa mazingira Sh, milioni 15 wamezitumia kununua Pikipiki Nane ambazo zitatumiwa na Maofisa Afya Mazingira.

Amesema fedha hizo hawakuona haja ya kuzitumia katika matumizi mengine, bali wazielekeze huko huko kwenye usafi wa mazingira, ili kuwapatia vitendea kazi maofisa afya na kuendelea kujituma zaidi kusimamia suala la usafi na kuendelea kuibuka washindi kila mwaka.

“Fedha hizi Shilinngi Milioni 15 ambazo tulizipata kwenye ushindi wa usafi wa mazingira mwaka jana kutoka Wizara ya afya tumeona tununu usafiri wa Pikipiki ili kuwawezesha Maofisa wetu Afya  na Mazingira wawe wanakagua usafi maeneo yote na mji wetu kuwa msafi muda wote,”amesema Satura.

“Mbali na Pikipiki hizi pia tumewapatia vyeti vya Pongezi wakiwamo na Watendaji wetu wa Kata ambao na wao hivi karibuni watapa Pikipiki lengo ni kuwatia moyo na kuwapa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii,”ameongeza.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amewataka Maofisa hao afya na mazingira kwamba mara baada ya kupewa Pikipiki hizo wasibweteke na kujisahau kufanya kazi, bali wakaendeleze kasi ile ile ya kusimamia usafi ili kuendelea kulinda ushindi wa usafi na wasitumie Pikipiki hizo kwa biashara ya Bodaboda.

Nao baadhi ya Maofisa hao afya na mazingira wameshukuru kupewa Pikipiki hizo na kuahidi kujituma kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha Mji wa Shinyanga unakuwa msafi muda wote.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akionyesha mfano wa Hundi Sh.milioni 15 ambayo walipewa mara baada ya kuwa washindi wa kwanza kundi la Manispaa katika Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, fedha ambazo wamenunua Pikipiki za Maofisa Afya Mazingira.

 Maofisa Afya Mazingira Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Pikipiki ambazo wamenunuliwa kupitia fedha za ushindi wa Tuzo ya usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya Sh.milioni 15.

 Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune (kulia) akikabidhi vyeti vya pongezi kwa Maofisa Afya Mazingira Manispaa ya Shinyanga pamoja na Watendaji wa Kata kutokana na kusimamia mazingira na kuwa safi.

 Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune (kulia) akiendelea kutoa vyeti vya pongezi kwa Maofisa Afya  Mazingira Pamoja na Watendaji wa Kata.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune (kulia) akibidhi cheti cha Pongezi kwa Mwakilishi wa Shirika la Mendeleo la Uholanzi SNV kutokana na mchango wao katika Manispaa ya Shinyanga kuimarisha masuala ya Usafi na Mazingira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post