SHUWASA YATOA ELIMU YA HUDUMA ZA MAJI KWA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI TOWN

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi shule ya msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakipatiwa elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), imetoa elimu ya huduma za maji kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga, huku ikiwataka wanafunzi wakawe mabalozi wazuri kwa wazazi, kutunza vyanzo vya maji na kulinda miundombinu ya mabomba.

Akizungumza wakati akitoa elimu hiyo leo Februari 24, 2023 katika shule hiyo ya Msingi Town
 Monica Paul Ndeha kutoka Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano kwa Umma SHUWASA, amesema wameamua kutoa elimu kwa wanafunzi, ili wakaisambaze majumbani mwao na kuwaeleza wazazi na walezi kile ambacho wamefundishwa kuhusiana na huduma za maji ambazo hutolewa na SHUWASA, ikiwamo na kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya mabomba.

“SHUWASA tumetoa elimu hii ya huduma za maji kwa wanafunzi shule ya Msingi Town, ili kuwapa uelewa juu ya huduma zetu, pamoja na kuwa Mabalozi wazuri wa kutunza nyanzo vya maji na kulinda miundombinu hasa mabomba,”amesema Ndeha.

“Naombeni wanafunzi elimu ambayo tumewapatia hapa mkawaambie na wazazi wenu, na mkiona mabomba yamepasuka toeni taarifa kwa watu wakubwa, ili na wao watupatie sisi taarifa na kuifanyia kazi na kudhibiti upotevu wa maji,”ameongeza Ndeha.

Naye Msaidizi wa Afisa Dira na Ankara kutoka SHUWASA, Justine Mbijuye, amewataka wanafunzi wanapokuwa shuleni au nyumbani wawe wanatumia maji vizuri na kutoyamwaga hovyo na kusababisha Ankara za maji kuja kubwa bali wawe na matumizi sahihi.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ya Msingi Town wameishukuru SHUWASA kwa kuwapatia elimu hiyo, hasa juu ya matumizi sahihi ya maji na kuacha kuyachezea hovyo.

Monica Paul Ndeha kutoka Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano kwa Umma SHUWASA, akitoa ya huduma za maji kwa wanafunzi shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga.

Fundi kutoka SHUWASA Uzia Bunyaga akitoa elimu ya huduma za maji kwa wanafunzi shule ya msingi Town Manispaa ya Shinyanga.

Msaidizi wa Afisa Dira na Ankra kutoka SHUWASA, Justine Mbijuye, akitoa elimu ya huduma za maji kwa wanafunzi shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga.

Msaidizi wa Afisa Dira na Ankra kutoka SHUWASA, Justine Mbijuye, akitoa elimu ya huduma za maji kwa wanafunzi shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji ambazo zinatolewa na SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza elimu ya huduma za maji kutoka SHUWASA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم