Mchungaji wa Kanisa la House on the Rock, Uche Aigbe ametiwa mbaroni na jeshi la polisi nchini Nigeria kwa kosa la kubeba bunduki aina ya AK-47 wakati wa mahubiri ya Jumapili wakati akitoa mahubiri kuhusu "silaha za kiroho".
Jeshi la polisi limethibitisha kumshikilia mchungaji huyo na ofisa mmoja wa polisi ambaye ndiye mmiliki wa bunduki hiyo.
Kwa mujibu wa kanisa lake, mchungaji Uche Aigbe awali aliomba msamaha kwa tukio hilo.
"Anatambua kwamba hata kwa nia nzuri, kubeba bunduki kuelezea ujumbe wake hairuhusiwi na ameonyesha kujutia kosa hilo," ujumbe wa Kanisa la House on the Rock liliandika katika taarifa yake iliyotoa kufuatia tukio la mchungaji huyo kuingia madhabahuni na bunduki.
Kanisa limeongeza kuwa linapinga aina zote za vurugu na linashirikiana kikamilifu na mamlaka wanapofanya uchunguzi wao kuhusu tukio hilo.
Sheria nchini Nigeria mtu yeyote haruhusiwi kubeba bunduki bila kupewa leseni na Inspekta Jenerali wa Polisi.
Social Plugin