Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIPONGEZA BARRICK BULYANHULU KWA KUFANIKISHA MIRADI YA KIJAMII SHINYANGA NA GEITA


Sehemu ya nyumba za walimu katika chuo cha VETA cha Bugarama zikiwa katika hatua ya Mwisho kukamilika,mradi wote wa VETA umegharimu shilingi milioni 961
Muonekano wa majengo ya sekondari la Igalula
Wakurugenzi wa TAMISEMI, Bw. John Cheyo- Sera na Mipango (kulia) na Vicent Kayombo-Elimu wakisikiliza taarifa ya miradi ya kijamii ya Barrick Bulyanhulu.
Kaimu Meneja wa Mahusiano ya jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii.
Mwonekano wa bweni la wasichana la shule ya sekondari Bugarama lililojengwa na fedha za CSR zilizotolewa na Barrick Bulyanhulu,pia imejengwa nyuma ya matron,vyumba vya madarasa na uzio.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwingiro, Antony Fabian akisoma risala kwa ujumbe wa TAMISEMI ulipotembea shule hiyo kuona maendeleo ya miradi ya fedha za uwajibikaji kwa jamii za Barrick Bulyanhulu.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango-OR-TAMISEMI, Bw,John Cheyo akitembelea moja ya wodi ya kituo cha afya cha Bugarama ambacho kimejengwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii za mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa Maofisa wa TAMISEMI na Barrick Bulyanhulu baada ya kutembelea kituo cha Afya cha Bugarama
 ****

Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, uliopo katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga umepongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya kijamii yenye kuboresha maisha ya wananchi kwa ufanisi mkubwa kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambayo tayari imeanza kuchochea kasi ya maendeleo katika maeneo hayo.



Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango-OR-TAMISEMI, Bw,John Cheyo, wakati alipoongoza ujumbe wa maofisa wa TAMISEMI kutembelea miradi ya afya na elimu iliyotekelezwa kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii zilizotolewa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika Halmashauri za wilaya ya Msalala na Nyang’hwale katika mikoa ya Shinyanga na Geita.


Bw.Cheyo, alisema amefurahi kuona miradi mbalimbali imekamilika na miundo mbinu ya elimu na afya imejengwa kwa viwango vya kuridhisha kwa kutoa huduma bora kwa Wananchi na kuchochea kufanikisha mipango ya Serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi hususani katika sekta ya elimu na afya.


“Nawapongeza Barrick Bulyanhulu na Watendaji wa Serikali kwa kusimamia ujenzi wa miradi hii na natoa wito kwa watumiaji wa majengo na vifaa vilivyonunuliwa mahospitalini kuvitunza ili vidumu na kuendelea kuhudumia wananchi wengi zaidi katika kipindi cha muda mrefu.


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mahusiano ya jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, alieleza ujumbe huo kutoka TAMISEMI kuwa miradi ikishapitishwa na halmashauri husika,mgodi unatoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kufanikisha mradi zinatolewa sambamba na kufanya ufuatiliaji kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango na muda uliopangwa.


Baadhi ya miradi mikubwa ambayo ujumbe huo ulitembea ambayo imejengwa kwa fedha za CSR za Barrick Bulyanhulu ni sekondari ya Mwingiro,Shule ya mchepuo wa kingereza ya Kharumwa,ujenzi wa madarasa na kuboresha maabara katika shule za sekondari za Kayenze, Igalula, Busulwangili,Bugarama,Chuo cha VETA Bugarama,chuo cha wauguzi cha Ntobo na kituo cha afya cha Bugarama.


Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwingiro, Antony Fabian akiongea kwa niaba ya wafanyakazi waliopo katika maeneo ya mradi na Wananchi alishukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Serikali kwa kufanikisha miradi hii mikubwa ambayo inaendelea kuboresha maisha ya wananchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com