Mwanamume mmoja ameshangaza mahakama ya Mombasa baada ya kukiri makosa ya udanganyifu wa kuilaghai kampuni ya bima ya Sh600,000 kwa kudanganya kuhusu vifo vya jamaa zake wa karibu.
Bw Philip Odero Kauma alighushi vifo vya binti yake, mama yake mzazi na mama mkwe wake kudai gharama za mwisho za heshima za kampuni ya moja ya bima.
Kulingana na hati ya mashtaka, mshukiwa alipata Sh.600,000 za Kenya (sawa na zaidi ya shilingi Milioni 11 za Kitanzania) kutoka kwa kampuni ya bima kwa madai ya uongo kwamba binti yake na mama yake walifariki dunia.
Alishtakiwa zaidi kwa kujaribu kupata Sh500,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 9 za Kitanzania kutoka kwa kampuni ya bima kwa kudanganya kifo cha mama mkwe wake.
Kesi hiyo itatajwa Februari 13.
Social Plugin