Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA TABIA YA KUFANYA MAZOEZI


Mbunge wa Jimbo la Malinyi Antipas Mgungusi akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya ushirika ambapo mbio za Kilimanjaro ndipo zilipo fanyika
Baadhi wa wananchi na wageni wakishiriki katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon.

Na Woinde Shizza , KILIMANJARO

Watanzania wametakiwa kutenga muda wao kwa ajili ya kufanya mazoezi kwani kwa kufanya hivyo kunawasaidia kuendelea kuwa na afya bora na njema pamoja kutenja afya zao na kuwaweka mbali na magonjwa .


Hayo yameelezwa na mbunge wa jimbo la Malinyi lililopo mkoani Morogoro Antipas Mgungusi ambaye pia ni muandaaji wa mbio za zijulikanazo kwa jina la Morogoro Marathon alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro wakati alipokuwa akishiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon ambapo alisema kuwa ni vyema kila mtanzania akajitaidi kutenga muda wake wa mazoezi kwa sababu mazoezi yanafaida kubwa mno ikiwemo na kuweka mwili na afya vizuri.


Alisema watu wengi hawana utaratibu wa kufanya mazoezi jambo ambalo sio zuri kiafya na hivyo kuwataka wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.


Aidha aliwapongeza waandaaji wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon kwa kuanzisha mbio hizo ambapo alisema kuwa mbio hizo zinasaidia sana mkoa huo kwani kwakufanya kipindi zinapofanyika zinasaidia kukuza pato la mkoa na la taifa kwa ujumla huku akibainisha kuwa mashindano hayo pia yanasaidia kuendelea kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi.


“Michezo ni muhimu sana kwa afya zetu … tujifunze na sisi tuanze kufanya mazoezi kwa sababu ni muhimu sana kwa afya zetu ,mimi hapa nilipo ni mwana michezo mzuri sana na nimekuwa nikishiriki mazoezi mara kwa mara na hii nikwaajili ya kuendelea kuboresha afya yangu niwasihi tu watanzania wenzangu wafanye mazoezi Sana kwani kwakufanya hivyo kunawasaidia hata kuepukana na magonjwa nyemelezi kama magonjwa haya ya pressure unaachana nayo,” alisema .


Aliongeza kuwa mbio kama hizi pamoja na mazoezi ya viungo kwa ujumla vinaimarisha afya ya mwili na akili na kuongeza ufanisi wa kazi, mara ambapo alifafanua kuwa mara nyingi baadhi ya watu wanafanya kazi wakiwa wamekaa na pia hawana muda wa kutosha wa kufanya mazoezi.


Aidha alimpongeza Rais Samia Suluhu kwa kuzindua filamu ya The Royal Tour na kubainisha kuwa filamu hiyo imeendelea kutangaza nchi ya Tanzania na hata katika mbio hizo faida yake imeonekana kwani kuna wageni walikuja kutokana na matangazo ya filamu hiyo lakini walivyofika na kuona mashindano hayo nao wakaamua kushiriki.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com