Madaktarii bingwa wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu wakifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye uti wa Mgongo ikiwa ni siku ya tatu ya kongamano la Kimataifa la Madaktari bingwa wa Ubongo,mgongo na Mishipa
Taasisi ya tiba ya Mifupa na Milango ya fahamu (MOI) imefanya Upasuaji mkubwa wa Kuondoa Uvimbe kwa kuingia kwenye uvungu wa Ubongo kwa Kutumia tundu za Pua za Mgonjwa pamoja na kufanya Upasuaji mwingine kwa mgonjwa aliyekuwa akisumbuliwa na Uvimbe kwenye Uti wa Mgongo.
Upasuaji huo umefanyika leo Februari 22 Jijini Dar es Salaam kwenye taasisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa mafunzo kwa Vitendo kupitia Kongamano la Kisayansi la Madaktari Bingwa na Wauguzi wa Ubongo na Milango ya Fahamu.
Akizungumza mara baada ya Kufanyika kwa Oparesheni hizo Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Milango ya Fahamu Dkt Nicephorus Rutabasibwa amesema mafanikio ya Upasuaji huo ni matokeo ya Jitihada za Serikali kuipa kipaumbele Sekta ya Afya kwa Kufanya uwekezaji mkubwa wa Vifaa tiba na vitendanishi.
"Tumewachagua wagonjwa waliokuwa na matatizo mbalimbali ambapo mgonjwa wa kwanza alikuwa na uvimbe kwenye kitezi cha Mgongo ambae dalili zake ilikuwa ni Kichwa kuumwa na baadae alipoteza kuona, lakini baadae tulipofanya vipimo tukakuta ana uvimbe kwenye Ubongo ambao unakandamiza mishipa ya fahamu ya kuona" amesema Dkt Rutabasibwa.
Kwa upande wake Dkt Laurent Mchome ambae pia ni Mbobezi wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu amesema Upasuaji uliofanyika leo sio mara ya kwanza Isipokuwa Utalaamu katika Upasuaji hubadilika mara kwa mara ndio ndio maana wameshirikiana na Wataalamu kutoka Colorado ili kufanya mafunzo ya pamoja ili kuongeza Ufanisi katika suala zima la Upasuaji hasa wa kuondoa Uvimbe kwa Wagonjwa wanaofika MOI kutibiwa.
" Tulianza kwanza kwa kujifunza Darasani ili tuangalie namna ya kushirikiana katika ujuzi ni mambo yamefika wapi sasa hivi, kwa sababu inawezekana Binafsi ninasoma na Daktari mwingine anasoma Binafsi lakini hatukutani pamoja ili kwenda pamoja lakini mikutano ya namna hii ni muhimu kwa sababu inatukutanisha pamoja Madaktari na hii inaleta tija zaidi" ameeleza Dkt Mchome
Madaktarii bingwa wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu wakifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kupitia kwenye pua, ikiwa ni siku ya tatu ya kongamano la Mwaka la Kimataifa la Madaktari bingwa wa Ubongo,mgongo na Mishipa likilenga kuwapa Wataalamu hapa nchini mbinu za kisasa za uchunguzi na matibabu ya uvimbe kwenye Ubongo na Mgongo ulioambatana na Saratani
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Milango ya Fahamu Dkt Nicephorus Rutabasibwa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo kuhusu operesheni waliofanya ya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kupitia kwenye pua pamoja na Uvimbe kwenye Uti wa Mgongo.
Dkt Laurent Mchome ambae pia ni Mbobezi wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu akizungumza na Waandishi wa habari akielezea upasuaji uliofanyika leo kwenye taasisi hiyo ya MOI na nama utaalamu ulivyotumika kwa kushirikiana na Madaktari bingwa kutoka sehemu nyingine.