SAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Sheikh mpya wa mkoa huo Sheikh Walid Alhad Omar amesema ameupokea uteuzi huo na kuahidi kumsaidia Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam tarehe 2 Februari 2023, Sheikh omar amesema anamuomba Mwenyezi Mungu amsaidie kutekeleza majukumu kutokana na uteuzi huo.
“Nimepokea uteuzi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir…namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie kutekeleza uteuzi huu uliokuja, lakini kama inavyojulikana lengo la uteuzi ni kumsaidia katika yale aliyopanga kusaidia jamii ya waislamu wa Tanzania na umma wote kwa ujumla.
“Namuomba Mwenyezi Mungu aniwezeshe kwa fadhila zake kukaimu nafasi hiyo,” amesema Sheikh Omar.
Social Plugin