Walengwa wa TASAF wakiwa na Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga wakipanda miti
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WALENGWA wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Mtaa wa Miti Mirefu Manispaa ya Shinyanga, wamepanda jumla ya miti 139 ya urembo (Royal Palm) kando kando ya barabara za mtaa huo, ili kutunza mazingira na kuupendezesha mji wa Shinyanga.
Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga, akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti leo Februari 24, 2023, amesema mradi huo wa upandaji miti ni mradi wa TASAF, ambapo walengwa wamepata ajira za muda mfupi na wamepanda miti hiyo ya urembo kwa urefu wa barabara kilomita 3.
Amesema zoezi hilo la upandaji miti kupitia mradi wa TASAF linaendana sambamba na agizo la Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango la kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka, na wametumia msimu wa mvua kupanda miti mingi.
“Mradi huu wa upandaji miti ni wa TASAF, na wanaopanda miti ni walengwa wenyewe, na wamepata ajira za muda na watapa pesa kupitia upandaji huu wa miti, na leo imepandwa jumla ya miti ya urembo 139 kwa ajili ya kutunza mazingira na kuupendezesha mji wa Shinyanga kwa sababu unaelekea kuwa jiji,” amesema Manjerenga.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya TASAF mtaa wa miti mirefu Said Juma, amesema Jumla ya Kaya za walengwa wa TASAF zipo 60, na wanapopanda miti hiyo kila baada ya siku 10 wanalipwa pesa Sh. 30,000 sawa na Sh.3000 kwa siku.
Nao walengwa hao wa TASAF akiwamo Catherine Mwikale, amesema mradi huo wa upandaji miti ni mzuri, kwa sababu unasaidia kutunza mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na pesa ambazo wanazipata kupitia upandaji huo miti zitawasaidia katika maisha yao.
Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akitoa elimu ya upandaji miti kwa walengwa wa TASAF.
Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akitoa elimu ya upandaji miti kwa walengwa wa TASAF.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la umwagiliaji maji miti likiendelea.
Zoezi la umwagiliaji maji miti likiendelea.