Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ameunda kamati kuwachunguza madaktari wa wilaya hiyo pamoja na mganga mfawidhi Halmashauri ya Mji Korogwe kwasababu za kuchelewa kufika kwenye tukio la ajali iliyouwa watu 20 Korogwe.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo jana, Jumamosi Februari 4, 2023 wakati akiongea na wafiwa waliokuwepo chumba cha kuhifadhia maiti Korogwe na kusema kuwa, lazima uchunguzi ufanyike kuhusiana na tukio la viongozi kushindwa kufika kwenye tukio.
"Itafanya uchunguzi wa kina kutokana na daktari wetu wa wilaya DMO na daktari mteule wa hospitali ya wilaya, sababu ya kuchelewa kufika eneo la ajali imetokea saa 4:30 usiku wao wamefika saa 10 kasoro." amesema Mgumba
Amesema kuwa ameunda kamati ambayo itawachunguza na kuwahoji mganga mkuu hospitali ya wilaya Korogwe pamoja na mganga mfawidhi hospitali ya Magunga Korogwe kufuatia kuchelewa kufika kwenye eneo la ajali.
Akiongea baada ya kutembelea eneo la ajali akiwa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga, ambayo ameambatana nayo hadi hospitali ya mji Korogwe ambapo ndipo ilipo hifadhiwa miili ya marehemu mkuu wa mkoa amesema.
Aidha mkuu wa mkoa pia akatoa maagizo kwa mganga mkuu wa mkoa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi hao huku pia akitoa wito kwa wananchi wa Korogwe na mkoa wa Tanga kutojihusisha na wizi wa mali pale inapo tokea ajali.
Social Plugin