Naibu waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mha.Methew Kundo.
Na Dotto Kwilasa, DODOMA
IKIWA ni maadhimisho ya siku ya usalama mtandaoni,Serikali imewekeza na kuwezesha fedha za kusimamia na kuratibu anga la mtandao salama huku ikiwataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya teknolojia ya mtandano ili taifa liendelee kuwa salama wakati wote.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhandisi Mathew Kundo ameeleza hayo Jijini hapa Katika maadhimisho hayo na kuongeza kuwa maadhimisho hayo yanatoa fursa na kutafakari juu ya mtandao salama na kuwataka Watanzania kuwa vinara katika ulinzi wa anga la mtandao.
Akiongea kwenye maadhimisho hayo amesema athari zinazotokana na mitandao zinaongezeka, maudhui potofu na unyanyasaji wa kijinsia hivyo ipo haja wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kushirikiana kuhakikisha anga la mtandao ni salama.
"Lazima tuwe walinzi,tuwafundishe namna bora ya matumizi sahihi ya mtandao hali itakayowezesha watoto na jamii kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na mtandao;
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini hadi Septemba 2022 idadi ya watumiaji wa mtandao walikuwa ni milioni 31.1 ambapo Tanzania mtandao umekuwa ukipatikana kwa gharma nafuu kuliko nchi nyingine,” alisema,"amefafanua
Amesema Watanzania wanatakiwa kuendelea kuwa vinara kushiriki katika ulinzi wa anga la mtandao na kwamba Serikalki imejipanga kuandaa mazingira bora na wezeshi yanayowezesha utoaji huduma za jamii, kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa na kuongeza uwazi na hata katika uchakataji ajira kupitia mtandaoni.
"Maendeleo yoyote ya teknolojia huja na faida zake na huwa na changamoto mbalimbali za usalama ikiwemo utapeli, unyanyasaji wa kijinsia na wizi wa utambulisho ni jukumu letu kujiandaa tunachokwenda kufanya kwenye mtandao kabla ya kuingia, bila tahadhari utaingia kwenye mambo ambayo hukutarajia,"amesema Kundo.
Aidha Naibu huyo Waziri mwenye dhamana ya mawasiliano amesema kila mtanzania ana wajibu wa kujua haki zake katika mtandao ili asivunje sheria.
"Kupitia kauli mbiui ya mwaka huu ni wezesha watanzania kwa mtandao salama,sisi kama Serikali tutaendelea kushirikiana na wadau wote juu ya anga mtandao ili kuwezesha kuilinda mifumo juu ya uharifu wa mtandao,"amesema
Kwa upande wake mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Irene Kabwili amesema kuwa siku ya usalama mtandaoni imekuwa ikitumika kwa kuendesha majadiliano ya pamoja na kwamba kuwepo kwa sera pekee haitoshi kila moja anatakiwa kuhakikisha anatumia mitandao bila kuvunja sheria.
Amesema kuwa Serikali kupitia Mamlaka hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu na kuhamasisha matumizi salama ili kubaini madhaifu yaliyopo na kuchukua hatua stahiki ili kuongeza ujuzi na weledi katika kukabiliana na matukio ya uhalifu mtandaoni.
Social Plugin