Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSIGWA AELEZA SABABU MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI KUSHINDWA KUWASILISHWA BUNGENI


Na Dotto Kwilasa, DODOMA

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo Gerson Msigwa ameeleza kushindwa kuwasilishwa kwa Muswada huduma za habari  Bungeni kuwa kumetokana na ufinuyu wa muda wa shughuli za bunge zinazoendelea hapa Jujini Dodoma.

 Msigwa amesema hayo kwenye Mkutano wake na Waandishi wa Habari, leo Februari 07, 2023, Saa 10:30 Jioni,katika Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO, Dodoma na kufafanua kuwa wabunge kujadili taarifa ya kamati za kudumu za bunge imepelekea kusogeza mbele  mswada wa Sheria ya huduma ya Habari uliofanyiwa marekebisho kutopelekwa bungeni kujadiliwa kama  ilivyo stahili .

Msigwa amesema kuwa Serikali ilikusudia kupeleka mswada wa Sheria ya Huduma ya Habari katika bunge ambalo linaendelea ili uweze kujadiliwa lakini kutokana na muda kuwa mfinyu hawakuweza kuwasilisha muswada huo na badala yake utawasilishwa katika bunge lijalo ambalo linatarajiwa kuwa mwezi wa nne.

Msemaji huyo wa Serikali amefafanua,"Kama mnavyojua ndugu zangu wana habari Serikali baada ya kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wa habari walitaka sheria ya huduma ya habari kufanyiwa marekebisho na kweli serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hasani aliona ni jambo jema ili kila mmoja aweze kufurahi na huduma hiyo,"amesema na kuongeza;

"Kweli serikali imekusanya maoni na hata wanahabari walitoa maoni yao kwa kutokana na kupatikana mwa maoni Serikali ilikuwa imekusudia kupereka marekebisho hayo bungeni ili wabunge waweze kujadili mswada huo,"anasisitiza Msigwa.

Pamoja na hayo amesema  bunge linaloendelea ni kwa ajili ya kujadili taarifa za kamati za bunge na kwa maana hiyo muda haukuweza kutosha kuweza kujadili muswada huo na kwamba mswada huo mahusu hautaweza kupelekwa bungeni kwa Sasa na badala yake utajadiliwa bunge lijalo la mwezi wa nne .

"Mswada huo utapelekwa bungeni na utajadiliwa kwani uko vizuri na umeandaliwa vizuri,maoni yote ya wadau yamezingatiwa na yamefanyiwa kazi tunataka mswada huo uweze kuwafurahisha watanzania wote ili kila mdau wa habari aweze kuwa na uhuru wa sheria hiyo na hiyo ndiyo makusudi njema ya serikali" amesema Msigwa .

"Pamoja na Sheria ya huduma ya Habari bado kuna miswada mingi ambayo ilitakiwa kupelekwa bungeni lakini kutokana na ufinyu wa muda miswada hiyo haikuweza kupelekwa bungeni na yote itapelekwa bungeni katika bunge ljalo  kwa manufaa ya watanzania wote,hii haiwezi kuathiri kitu chochote,"amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com