Mwanafunzi wa shule ya upili nchini Ufaransa amemuua kwa kumchoma kisu mwalimu mmoja raia wa Uhispaniaa katika shule moja katika mji wa Saint-Jean-de-Luz nchini Ufaransa.
Msemaji wa serikali ya Ufaransa Olivier Véran amethibitisha shambulio hilo la Jumatano ya leo na kusema mhusika ana umri wa miaka 16.
Polisi wamefika katika shule ya Saint-Thomas d'Aquin na mwendesha mashtaka wa eneo hilo, ambapo mwanafunzi huyo alikamatwa. Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kwamba mshambuliaji huyo aliingia darasani wakati mwalimu huyo wa Uhispania akitoa darasani na kumshambulia kwa kisu.
Mwalimu huyo anayekadiriwa kuwa na na umri wa miaka 50 alifariki kutokana na mshtuko wa moyo baada ya huduma za dharura kuwasili shuleni hapo, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Inasemekana mshambuliaji huyo alifunga mlango wa darasa na kumdunga kisu mwalimu huyo kifuani mwake.
Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Pap Ndiaye ameelekea mara moja shuleni hapo.