NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imezindua jezi zao mpya ambazo zitatumika kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambazo kifuani kutakuwa na neno Visit Tanzania.
Akizungumza katika tukio hilo leo Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa hiyo Ahmed Ally amesema Jezi zitauzwa shilingi elfu 35,000 kwa jezi moja na zitaanza kuuzwa Februari 15, 2023 na wachezaji wataanza kuvaa wakienda kucheza na Horoya.
"Tukisafiri tutakuwa na M-Bet, siku moja kabla ya mechi na siku ya mechi ndio tutakuwa tunatumia Visit Tanzania kama ilivyo matakwa ya CAF." Amesema Ahmed Ally.
Kwa upande wake Mdhamini wa Klabu hiyo Bw.Adom Mgoyi ameseishukuru Bodi ya Utalii kwa kuwaruhusu kutumia neno Visit Tanzania ili kuitangaza nchi kwani historia ya Simba ni kubwa na ndio klabu pekee nchini ambayo inaweza kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi."
"Lakini pia tunamshukuru mwekezaji wetu Mohammed Dewji kwa kazi kubwa anayoifanya. Pia nichukue nafasi hii kuwapongeza watu wote walioshinda kwenye uchaguzi wa Simba". Amesema Mgoyi.
Social Plugin