Zaidi ya watu 8,700 wanadaiwa kufariki nchini Uturuki na Syria kufuatia tetemeko la ardhi la Jumatatu. Idadi ya vifo nchini Uturuki imeongezeka hadi 6,234, kwa mujibu wa shirika la maafa nchini humo.
Ni vigumu kuthibitisha idadi hiyo nchini Syria, lakini vyombo vya habari vya serikali vinasema takriban watu 2,500 wameuawa.
Kundi la uokoaji la White Helmet, ambalo linahudumu katika eneo linalodhibitiwa na waasi, linasema idadi ya waliouawa imeongezeka hadi zaidi ya 1,280.
Social Plugin