Basi la mwendokasi lililopata ajali
Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kwamba imepokea majeruhi 37 wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea hii leo Februari 22, 2023 na kwamba haijapokea kifo chochote.
Aidha taarifa zaidi kuhusu mtembea kwa miguu aliyegongwa na basi hilo itatolewa baadae.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam, bwakati basi la mwendokasi likitaka kulikwepa gari dogo na kupelekea kugonga ukuta.
Social Plugin