Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited-Australia Henk Diederichs jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023. Kampuni ya ORECORP Limited imeingia ubia na kampuni ya Sotta Mining Limited yenye ubia na serikali kuchimba dhahabu eneo la vijiji vya Sotta na Nyabila vilivyopo Igalula Sengerema mkoani Mwanza.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited – Africa Damien Valente akizungumza wakati wa kikao baina ya uongozi wa ORECORP Limited na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023.
Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha akizungumza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited- Australia Bw. Henk Diederichs (kushoto) na Meneja Mkuu Sotta Mining Corporation – Afrika Bw. Damien Valente (katikati) wakati Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula alipokutana na uongozi wa ORECORP Limited tarehe 14 Februari 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa tatu kulia) akiwa katika picha na ujumbe wa kampuni ya uchimbaji madini ya Nyanzaga pamoja na Wizara ya Ardhi walipokutana jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)
**************************
Na Munir Shemweta, WANMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited Bw. Henk Diederichs.
Mazungumzo baina ya Waziri Dkt Mabula na Mtendaji Mkuu huyo wa ORECORP Limited yamefanyika jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha.
Kampuni ya ORECORP Limited imeingia ubia na kampuni ya Sotta Mining Limited yenye ubia na serikali na kuunda kampuni ya uchimbaji madini ya Nyanzaga Mining Corporation Limited ambapo Sotta Mining Corporation inamiliki asilimia 84 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki asilimia 16.
kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Nyanzaga inatarajia kuchimba dhahabu eneo lenye ukubwa wa 23.36 kilometa za mraba lilipo vijiji vya Sotta na Nyabila kata ya Igalula wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayotumiwa na mgodi huo ambapo ili kampuni hiyo kuanza shughuli zake inatakiwa kutwaa ardhi kwa mujibu wa sheria kwa kuhakikisha wananchi wanalipwa fidia stahiki na kupisha katika eneo hilo.
Kampuni ya uchimbaji dhahabu Nyanzaga ilitoa kandarasi kwa kampuni ya Uthamini ya Ace Consultants LTD ya kutekeleza zoezi la uthamini wa mali za wananchi wanaotakiwa kupisha shughuli za uchimbaji.
Social Plugin