WAZIRI MCHENGERWA KUPOKEA MAGEUZI MATATU YA KIHISTORIA FEBRUARI 3,2023


*************************

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kupokea Mageuzi matatu ya kihistoria katika wizara hiyo siku kesho Februari 03,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 02,2023 Ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa na Utamaduni Dkt.Hassan Abbas amesema Wizara hiyo siku ya kesho inaenda kuandika historia kubwa 3 zenye mchango mkubwa kwa taifa la Tanzania.

"Ni lazima nchi ya Tanzania tuwe na Muziki ambao unalimtambulisha taifa hivyo tuliteua kamati ambayo iliongozwa na watu wabobezi katika kuhakikisha mdundo unapatikana kwa kuzingatia mdundo huo haupotezi vionjo vya kitamaduni ya kitanzania."

Hata Katibu mkuu ameeleza kuwa Kamati hiyo ilisheheni watayarishaji mbalimbali na wadau wakubwa wa Kimuziki.

"Kamati hii iliongozwa na Mwenyekiti Dkt.Kedmon Mapana nafikiri umahiri wake unafahamika ,Masoud Masoud manji wa muziki, Master jay,dj fetty pamoja na p funk na wengine. "

Aidha, amesema kuwa waziri pia atapokea Jambo la pili ambalo ni kupokea taarifa ya Vazi la taifa ambalo limekuwa ni mchakato wa muda mrefu kupatikana lakini taifa litakwenda kupokea rasmi taarifa ya mchakato wa vazi hilo .

"Baada ya Majadiliano ya muda mrefu wizara inaenda kupokea mapendekezo ambayo wadau wametoa na kushauri namna ya vazi la taifa liweje."

Hata hivyo amesema vazi hilo litakuwa vazi la heshima na litakalovaliwa katika matukio muhimu zaidi.

Pia Katibu Mkuu ameongeza kuwa jambo la 03 litakalofanyika kesho ni pamoja na utoaji wa mikopo kwa awamu ya pili kwa wasanii ambao wamekidhi vigezo vya kukopeshwa fedha kwenye mfuko wa Utamaduni ya Maendeleo ya Sanaa.

"Kuna vipawa vingi kwenye sekta yetu ya Sanaa inapelekea wasanii wengi kutoweza kufanya kazi zao vizuri kutokana na kukosekana kwa fedha hivyo mfuko huo utaenda kuwawezesha wasanii wa kitanzania na Mfuko huo utakabidhi mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1 za Kitanzania. "

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post