Madaktari nchini Kenya wamemfanyia upasuaji Bi. Felister Namfua (36) na kutoa wembe wa upasuaji uliosahaulika ndani ya tumbo kwa muda wa miaka 11.
Bi Felister amekua akiishi na maumivu makali ya tumbo kwa miaka 11 akiamini kuwa ana vidonda vya tumbo (ulcers) na amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo.
Tatizo hilo lilianza wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza katika hospitali ya Kitale Magharibi mwa Kenya.
Kadri miaka ilivyozidi kwende, aliendelea kupata maumivu makali, ndipo madaktari walipata shauku kuwa ugonjwa alionao ni mkubwa kuliko vidonda vya tumbo.
Mume wa Felister Stephen Mungai ameomba vyombo vya usalama nchini humo kuchunguza madaktari wamliofanyia upasuaji mke wake huku akidai fidia kutokana na matatizo waliomsababishia.
Social Plugin