Na Dotto Kwilasa, DODOMA
Hatua hiyo ni kufuatia mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Bunda Vijijini (CCM), Mwita Getere kudai kumekuwa na minong’ono kuwa kutotangazwa kwa mpangilio wa ufaulu kunadhoofisha elimu ya Tanzania.
Mbunge huyo amehoji ,"Kwa kuwa Serikali imo humu ndani kwanini isitoe taarifa humu ndani kipi bora, hayo matangazo waliyositisha yana umuhimu gani kwa wananchi na yana ubora gani kwa wananchi,”
Akijibu mwongozo huo leo Bungeni Profesa Mkenda amesema,"Chukua shule ambayo ina watoto 100, nyingine ina wanafunzi 20, wamemaliza kidato cha nne, wanafunzi 170 wapata alama A, 30 hawakupata A, wenye wanafunzi 20 wote wamepata A kwa kuangalia wastani ufaulu ni wazi wenye wanafunzi 20 itatangazwa ni shule bora.
“Wengine watasema shule ya wanafunzi 70 wakapata A si bora zaidi, kuliko shule ya wanafunzi 20 tu. Ukiacha aina hiyo ya tathimini inaweka shinikizo kwa shule ya wanafunzi 100 kwa mfano kuhakikisha inawaondoa wale 30 waweze kutangazwa shule bora”, amesema.
Prof.Mkenda ameema , kuna njia tatu zinaweza kutumika kufanya tathmini ikiwa ni pamoja na kuangalia matokeo ya mwisho ya mitihani kama iliyokuwa ikifanywa na NECTA na kwamba tatizo la njia hiyo haisemi shule imechangia nini katika maendeleo ya mtoto husika.
"Njia hiyo imeacha kutumiwa na nchi nyingi duniani na badala yake wanatumia nyongeza ya thamani (value edition) kwa kuangalia mwanafunzi alianza akiwa vipi na shule imechangia nini katika kumwinua mtoto katika masomo yake," amefafanua.
"Kwa maana hiyo shule bora inaweza kuwa ya kata tu, imechukua wanafunzi wanaoonekana wa wastani lakini wanapomaliza ile shule ikawa na matokeo mazuri kwa kuongeza ubora wa wanafunzi kuliko ile inayochagua wanafunzi bora tu,”amesema.
Kuhusu njia ya tatu amefafanua kuwa si kwamba inaangalia mtoto aliingiaje shuleni bali na mazingira yake yakoje na kutolea mfano shule iko katika mzingira magumu maji hayapatikani karibu, hakuna mabweni na jamii masikini.
"Njia hiyo inaangalia japo mazingira hayo magumu lakini walimu wakafanya kazi na kuhakikisha mwanafunzi aliyeingia kwa wastani anapata daraja A,katika mazingira hayo, shule hiyo itakuwa imeongeza kikubwa kuliko mwenye historia ya kuchukua wanafunzi mwenye ufaulu wa juu na katika mitihani yake ya mwisho akapata ufaulu mkubwa," amesema.
Amesema tathimini hiyo inahitaji wataalam wa takwimu na kwamba watakapokuwa na tathimini hiyo ndio wanaweza kuwaambia wazazi kuwa shule ipi ni bora.
Amesema hawajazuia mtu yoyote kusema shule ipi ni bora na kwamba matokeo yapo katika mtandao na Serikali haijaficha hilo na kusisitiza kuwa baraza halichukui kutangaza matokeo ambayo kisayansi yamelaumiwa na wataalam wa elimu.
Hata hivyo amesema huko mbele baraza litaangalia namna nzuri ya kupangilia mambo hayo yote na kwamba Wizara haiwezi kuondoa ushindani na ndio maana imeweka madaraja.
Social Plugin