ZAO LA MPIRA KUENDELEZWA MAENEO YENYE HALI YA HEWA INAYOKUBALIKA NCHINI


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiongea na Wafanyakazi wa Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro alipotembelea Shamba hilo Februari 11, 2023

Wafanyakazi wa Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) alipokuwa akiongea nao alipotembelea Shamba hilo Februari 11, 2023

Msimamizi wa Shamba la Kalunga Bwana Egata Makanja akiwlezea hali ya hewa inayofaa kwa kilimo cha mpira kwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) alipotembelea Shamba lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro. Februari 11, 2023


Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hashil Abdallah (kulia) akimueleza Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) (Kushoto) mpango wa NDC wa kuondoa miti iliyozeeka na kupanda mipya kwa kizingatia kupata faida zote za miti hiyo ikiwemo mpira, mbao na hewa ya ukaa Walipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro Februari 11, 2023



Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) (Katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hashil Abdallah (Kushoto) wakiangalia Mpira uliochakatwa baada ya kugemwa Walipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro Februari 11, 2023 kuangalia jitihada za kuliendeleza zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).


Mpira uliochakatwa na kuanikwa katika Shamba la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe Walipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro Februari 11, 2023 wakiangalia mbegu za miti ya Mpira inayoandaliwa kwa ajili ya kupandwa.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) (Katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hashil Abdallah (Kushoto) pamoja na wakimbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kilombero Mpira Walipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero, Morogoro Februari 11, 2023 kuangalia jitihada za kuliendeleza zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC)

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ametoa wito kwa wakulima walioko katika maeneo yenye hali ya hewa kama ya Mang’ula Kilombero kulima zao la Mpira ili kukidhi mahitaji ya soko la 99.7% ambalo kwa sasa mauzo ya zao hilo ni 0.03%

Waziri Kijaji ameyasema hayo Februari 11, 2023 alipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro kuangalia jitihada zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) katika kuendeleza uzalishaji wa zao hilo la Mpira ambalo ni zao la kimkakati linalotumika kutengeneza bidhaa kama matairi, magodoro na gloves.

Dkt Kijaji pia ameitaka NDC kuelimisha umma kuhusu uzalishaji wa zao hilo huku akizitaka SIDO na TEMDO kutengeneza mashine zitakazowawezesha wakulima hao kuchakata zao hilo kwa gharama nafuu ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya ujenzi wa uchumi jumuishi wa viwanda.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah alieleza kuwa NDC imeweka utaratibu wa kuondoa miti ya zamani iliyopandwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Kwanza mwaka 1978 na imeisha muda wake na kupanda mpya ili kuhakikisha miti hiyo inatoa faida iliyokusudiwa ya mpira, mbao, kuni na utunzaji wa mazingira kwa utoaji wa hewa ya ukaa.

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema NDC imejipanga kupanda miche laki mbili ya mpira na inakamilisha taratibu za kuthibitishwa kuwa mzalishaji na msambazaji wa mbegu za zao la mpira ili kuhamasisha wananchi kulima zao hilo nchini na kukidhi mahitaji makubwa ya soko ndani na nje ya nchi

Vilevile, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bw. Christopher Wangwe ameahidi kuongeza eneo la shamba la Kalunga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mlimba na amepanga kila shule kupanda miche 50 na kila mwanafunzi apande mche mmoja nyumbani ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo linalotoa malighafi za viwandani na kuongeza ajira katika halmashauri hiyo.

Naye, Msimamizi wa Shamba Bwana Egata Makanja amesema zao hilo linaweza kustawi katika mazingila yenye mvua kati ya milimita 2000 hadi 2500 nyuzi joto 20 hadi 35 auwastani wa 27 na unyevunyevu 80% na mwanga wa jua wa masaa 2000 kwa mwaka na linaweza kupandwa na mazao mengine ya chakula mwanzoni nahuanza kuvunwa likiwa na miaka mitano kwa kipindi cha miaka 30

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post