Mazishi ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Richard Makore aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Nipashe Kanda ya Ziwa yamefanyika nyumbani kwake Kijiji cha Remong'orori Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Ijumaa Machi 10, 2023.
Makore aliyezaliwa mwaka 1978 alifariki Jumanne Machi 07, 2023 katika ajali ya basi la Sheraton iliyotokea katika eneo la Kasamwa mkoani Geita likitokea jijini Mwanza na kusababisha jumla ya vifo 10 na majeruhi kadhaa.
Mauti yalimkuta Makore akiwa safarini akielekea kwenye majukumu ya kikazi mkoani Geita.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Social Plugin