Watu 14 wamefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabara ambayo imehusisha basi la chuo kikuu.
Basi la Chuo Kikuu cha Pwani limegongana na matatu katika eneo la Kayole Naivasha kaunti ya Nakuru.
Wanafunzi wa chuo hicho pamoja na wahadhiri ni miongoni mwa waliohusika kwenye ajali hiyo.
Ripoti zinasema basi hilo lilikuwa na takriban wanafunzi 30 ambao walikuwa wakielekea Eldoret katika chuo kimoja kuhudhuria michezo.
Kiini cha ajali hiyo hakijabainika ila walioshuhudia wanasema ilitokana na kufeli kwa breki za basi hilo.
Baada ya hiyo kufanyika basi liligongana na matatu ya abiria katika eneo hilo la Kayole barabara ya Nairobu-Nakuru.
Social Plugin