Naibu Waziri wa madini,Dk.Stephen Kiruswa, akiongea na wafanyakazi wa Barrick wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye mkutano wa jukwaa la pili la utekelezaji wa ushirikishwaji watanzania katika sekta ya madini unaondelea katika ukumbi wa AICC mjini Arusha leo (kulia) ni Meneja wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido na wengine ni maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Madini.
Wafanyakazi wa Barrick wakibadilishana mawazo katika banda la maonesho lililopo katika ukumbi wa AICC mjini Arusha.
Wafanyakazi wa Barrick wakibadilishana mawazo katika banda la maonesho lililopo katika ukumbi wa AICC mjini Arusha.
Wafanyakazi wa barrick wanaoshiriki mkutano wa jukwaa la pili la utekelezaji wa ushirikishwaji watanzania katika sekta ya madini wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido,( wa tatu kutoka kulia).
***
Naibu Waziri wa madini Dk. Stephen Kiruswa, ameipongeza kampuni ya uchimbaji wa dhahabu wa Barrick kwa utekelezaji wake wa sera ya ushirikishaji watanzania katika mnyororo wa sekta ya madini kwa vitendo.
Dk. Kiruswa, akiongoza ujumbe wa Maofisa Waandamizi kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini walitembelea banda la maonesho la kampuni ya Barrick na Twiga lililopo kwenye mkutano wa jukwaa la pili la utekelezaji wa ushirikishwaji watanzania katika sekta ya madini unaondelea katika ukumbi wa AICC.
Ujumbe huo wa Naibu Waziri Kiruswa ulipatiwa maelezo kuhusiana na jinsi Barrick inavyotekeleza sera hiyo na jinsi inavyoendelea kuwanufaisha Watanzania wanaofanya biashara na migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara ,ambapo aliipongeza Barrick kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza sera hiyo.
Social Plugin