Mgombea wa chama tawala Bola Tinubu ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata nchini Nigeria.
Mpinzani wake mkuu Atiku Abubakar alipata 29%, na Peter Obi wa Labour 25%. Vyama vyao hapo awali vilitupilia mbali uchaguzi huo kama udanganyifu, na kutaka marudio.
Bw Tinubu ni mmoja wa wanasiasa tajiri zaidi wa Nigeria, na aliegemeza kampeni yake kwenye rekodi yake ya kujenga upya jiji kubwa zaidi la Lagos alipokuwa gavana.
Hata hivyo alishindwa mjini na Bw Obi, mgeni ambaye alihamasisha uungwaji mkono wa vijana wengi hasa wa mijini, na kutikisa mfumo wa vyama viwili nchini.
Bw Tinubu alishinda majimbo mengine mengi katika eneo alikozaliwa la kusini-magharibi, ambako anajulikana kama msuka mipango na mfadhili mkuu wa siasa (godfather) za Nigeria
Alifanya kampeni ya urais chini ya kauli mbiu: "Ni zamu yangu".
Rais Muhammadu Buhari anaondoka baada ya mihula miwili madarakani, inayoashiria kudorora kwa uchumi na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama nchini humo - kutoka kwa waasi wa Kiislam kaskazini-mashariki hadi mzozo wa kitaifa wa utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi na mashambulio ya kujitenga kusini-mashariki.
Bw Tinubu sasa ana jukumu la kutatua matatizo haya, miongoni mwa mengine, katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika na muuzaji mkubwa wa mafuta nje ya nchi.
Baada ya kukabiliana na utawala wa kijeshi nchini Nigeria, kutorokea uhamishoni na kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa demokrasia ya nchi hiyo mwaka wa 1999, Bw Tinubu atahisi kwamba alikusudiwa kuwa rais.
Siku zote alikuwa anapendelea kuchukua nafasi ya Bw Buhari - ambaye alimsaidia kuwa rais - na vikwazo ambavyo amevuka hadi kufika hapa vitafanya ushindi huu kuwa mtamu zaidi kwake.
Hakutarajiwa kushinda mchujo wa chama, lakini alishinda.
Wengi walisema uamuzi wake wa kwenda na Mwislamu mwingine kama mgombea mwenza ungekuwa kikwazo, lakini haikuwa hivyo.
Sasa itabidi athibitishe kwamba anaweza kupiga hatua na kwamba bado ni nguvu ile ile ya kutisha iliyojenga Lagos ya kisasa, kitovu cha kibiashara cha Nigeria.
Bw Tinubu atasimamia uchumi unaoporomoka, ukosefu wa usalama ulioenea na kama ramani ya matokeo inavyoonyesha, nchi inayojitoa katika kambi za kikanda na kidini.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin