Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) umetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ)kuhusu mradi wa Boresha Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ili kuhakikisha Waandishi chipukizi wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati wanakuwa na uelewa hasa kwenye masuala ya usawa wa kijinsia pamoja na uandaaji wa Bajeti yenye mrengo wa kijinsia wakati wa uandishi pamoja pamoja na kuripoti habari mara baada ya kuhitimu masomo yao.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo leo , Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Mariam Oushoudada amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) wanapata elimu ya kutosha kuhusu masuala ya uandishi wa habari wa Kijinsia pamoja na kujua jamii kwa ukaribu zaidi hasa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu kabla hawajaanza kuripoti habari.
Amesema lengo ni kuweza kuwainua wanawake kwenye masuala yote ya uongozi pamoja na kujitambua kwani wanawake wengi bado hawana ujasiri wa kuwania nafasi kwani bado hawajapewa elimu ya kutosha hivyo mradi huo umekuja kwenye wakati mzuri hasa kwa wanachuo wa wanaosomea tasnia hiyo kwani watakuwa mabalozi wazuri.
Pia amesema Vyombo vya habari vingi haviripoti habari nyingi za masuala ya kijinsia hivyo kuamua kufanya mafunzo kwa wana habari waliopo vyuoni itaweza kuleta hamasa na kutambua umuhimu wa habari zenye mrengo wa Kijinsia kwenye jamii inayowazunguka.
Naye Mwanafunzi wa Diploma ya Habari kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) Nura Mohamed amesema habari za masuala ya kijinsia wanazisikia mara chache hasa kwenye Uandishi hivyo kutokana na mafunzo hayo itawasaidia wanapokwenda kufanya kazi za Uandishi wa Habari wataweza kuzipa kipaumbele kwani ndiyo ngao kwa jamii.
Amesema hapo mwanzo wanafunzi wengi hawakuwa na uelewa zaidi kwenye Uandishi wa Habari za kijinsia hivyo mradi wa Boresha Habari utakuwa chachu kwao pale watakapokuwa wanaandika habari za masuala ya kijinsia kwani jamii nyingi za hapa nchini hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kijinsia.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za kijinsia pamoja uandaaji wa Bajeti yenye mlengo wa kijinsia kazi zinazofanywa na mtandao huo wa Jinsia kwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) wakati wa mafunzo ya mradi wa Boresha habari yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Mariam Oushoudada akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) waliofika kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushiriikiana na chuo hicho.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Esther William akitoa maelezo kuhusu namna mtoto wa kike anavyoweza kijisimamia pamoja na kazi zinazofanywa na huo mtandao wa Jinsia kwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) wakati wa mafunzo ya mradi wa Boresha habari yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) waliofika kwenye mafunzo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatole na watoa mada kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) hasa kwenye masuala ya kijinsia wakati wa mafunzo ya mradi wa Boresha Habari yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Social Plugin