Mtangazaji wa Clouds TV, Sakina Lyoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani uliofanyika katika Chuo cha Practical School of Journalism kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu masuala ya usawa kijinsia kwa wanafunzi wa Chuo cha Practical School of Journalism kwenye uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari uliofanyika katika chuo hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Esther William akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja pamoja na maswali yaliyokuwa yanaulizwa wakati wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari
Mkufunzi kutoka Chuo cha Practical School of Journalism akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kuweza kuzindua mradi wa Boresha Habari.
Baadhi ya wanafunzi wakufuatilia mada kwenye uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari
***
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umezindua mradi wa Boresha Habari katika vyuo vya uandishi wa habari kuhamasisha uandishi wenye mrengo wa kijinsia.
Akizungumza leo Jumatano Machi 8,2023 wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Boresha Habari kwenye Chuo cha Practical School of Journalism, Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba amesema TGNP inapenda kuona waandishi wa habari ambao bado hawajaingia kwenye vitendo wanaelewa vizuri masuala yote ya usawa wa Kijinsia pamoja na kujua uandishi wa habari wa Kijinsia pamoja na kuijua jamii kwa ukaribu zaidi hasa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu.
Pia amesema lengo ni kuona waandishi hao wanaandika makala au habari zinazohusiana na masuala yenye mrengo wa Kijinsia kwa kwa kuweka kwenye mitandao ya kijamii ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
"Bila kuwa na waandishi wa habari wazuri wanaojua masuala ya usawa wa Kijinsia hatuwezi kuwa na maendeleo mazuri hivyo uzinduzi wa mradi huo kwenye Chuo cha Practical School of Journalism ili kuanza mafunzo kwenye chuo hicho yanayohusiana na Masuala yenye mrengo wa Kijinsia", amesema Temba.
Social Plugin