MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH),Dk Alphonce Chandika,akizungumza wakati akielezea miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital hiyo leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH),Dk Alphonce Chandika,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital hiyo leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
BALOZI wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yusushi Misawa,akizungumzia ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Japan wakati wa mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Shonan Kamakura General Hospital Prof.Shuzo Kobayashi,akizungumzia mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Taasisi ya Tokushukai Dkt. Higashiue Shinichi,akizungumzia mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Figo Chuo Kikuu cha Dodoma na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Alfred Meremo,akizungumzia wakati wa mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
DAKTARI Bingwa Magonjwa ya Figo Hospitali ya Benjamin Mkapa Dk.Kessy Shija,akielezea magonjwa ya figo wakati mtu anapotaka kusaidiwa Figo wakati wa mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka,akizungumza wakati wa mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
Mdau wa Sekta ya Afya Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati wa mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH),Dk Alphonce Chandika,akimkabidhi Cheti ya ushirikiano Mwenyekiti wa Taasisi ya Tokushukai Dkt. Higashiue Shinichi, wakati wa mafanikio ya miaka mitano ya Upandikizaji figo katika hospital hiyo leo Machi 13,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
HOSPITALI ya Benjamini Mkapa imefanikiwa kupandikiza figo kwa wagonjwa 33 kati ya hao wagonjwa 22 wamepandikizwa na wataalamu wazawa.
Aidha imesema mtu anaechangia figo yupo salama na hapatwi na maradhi yoyote ambapo mpaka sasa wametoa figo za watu 33 ambao hawajapata madhara yoyote.
Hayo yameelezwa leo Machi 13,2023,Jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo,Dk Alphonce Chandika, wakati alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya miaka mitano tangu hospitali hiyo ilipoanza kupandikiza figo.
“Jambo hili limefanikiwa kwani mpaka sasa tumefanikiwa kupandikiza figo kwa wagonjwa 33 kati ya hao wagonjwa 22 wamepandikizwa na wataalamu wazawa.
“Ni furaha yangu kuwaambia kwamba kwa sasa wataalamu wetu wanafanya zoezi hili wao wenyewe bila ya kuwepo kwa usimamizi wa watu wa Japan haya ni mafaniko makubwa,"amesema Dk Chandika
Amesema gharama za matibabu ya figo nchini India na Duniani kote ni makubwa ambapo Serikali ya Tanzania itaweza kuokoa kutokana na kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwasababu huduma huyo kwa sasa inapatikana nchini.
Aidha Dk. Chandika amesema Serikali imeweka vifaa tiba na miundombinu ya kisasa kwa ajili ya kufanikisha huduma hiyo.
Amesema gharama ya kumpeleka mgonjwa kutibiwa India ni Sh kati ya milioni 77 hadi 80 kwa mgonjwa kufanyiwa upandikizaji ambapo kwa hapa nchini ni Sh milioni 35.
“Huu ni ugonjwa ambao mtu anatakiwa awe na fedha za kutosha kuanzia usafishaji wa damu ambayo ni hatua ya mwanzo kabla ya kufanya upandikizaji wa figo.
Amesema mgonjwa hutakiwa damu walau mara tatu kwa wiki ambayo humgharimu Sh 700,000 mpaka 900,000.
Aidha amesema Hospitali inahitaji kuwa na wataalamu wasiopungua 32 kwa upandikizaji mmoja ‘one pair’ wanaotokana na taaluma mbalimbali za eneo la upandikizaji figo.
Ameyataja maeneo hayo ni madaktari bingwa wa upasuaji,mabingwa wa magonjwa ya figo,mabingwa wa maabara,mabingwa wa usingizi,wauguzi wa upasuaji,wauguzi wa vyumba vya uangalizi maalum.
Wengine ni wataalamu wa mambo ya jamii,wataalamu wa lishe na ofisi inayoratibu zoezi zima la upandikizaji wa figo.
Amesema mpaka sasa,Hospitali ya Benjamini Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Tokushukai Medical Group wamefanikiwa kuwapatia mafunzo wataalamu 13 nchini Japan.
“Kwa miaka hii mitano tumegundua ama kujifunza kwamba wananchi wengi hatupo tayari kujitolea kuwachangia ndugu na jamaa zetu walio na maradhi ya figo wenye vigezo na uhitaji wa kupandikizwa,”amesema.
Dk. Chandika amesema kuwa mtu anaechangia figo yupo salama na hapatwi na maradhi yoyote kwa sababu ya kuchangia figo.
“Nasema haya kwa uhakika kabisa tuna watu 33 waliochangia figo kunusuru maisha ya ndugu zao hapa hospitali ya Benjamini Mkapa hakuna hata mmoja aliyewahi kurudi akiwa na shida inayotokana na kuchangia figo.
Amesema mipango ya muda mfupi ni kuboresha huduma za kupandikiza kwa kujenga miundombinu stahiki ambapo amedai tayari wamemaliza hatua ya michoro ili kutengeneza eneo maalum la kutolea huduma za kupandikiza figo.
''Tunakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu kupiga simu na kutaka kuuza figo zao ambapo ni kinyume na sheria za nchi ambapo ni kosa kwa mtu kuuza viungo vyake vya miwili', amesema Dk. Chandika.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Tokushukai Dkt. Higashiue Shinichi, amesema kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana vizuri ili kuhakikisha Benjamin Mkapa inapiga hatua katika suala la Upandikizaji figo kwa wagonjwa.
"Tunaishukuru serikali ya Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa BMH kwa kutuonyesha ushirikiano,tutaendelea kuwa pamoja ili kuimarisha wataalam wa mgonjwa ya figo," amesema Dk. Shinichi.
Social Plugin