Kulikuwa na hali ya sintofahamu baada ya hafla ya harusi kukatizwa ghafla bibi harusi alipogundua kwamba bwana harusi ni baba wa watoto saba.
Inasemekana kuwa bibi harusi alikataa kuendelea na karamu hiyo baada ya kutambua kuwa bwana harusi hakuwa mwaminifu kwake, kwani alimficha kuhusu kuwa na familia nyingine.
Video ya haflla hiyo iliyopakiwa mitandaoni yaonyesha eneo la karamu hiyo katika jimbo la Benin, Nigeria likiwa limepanguliwa huku viti vikiwa vimetapakaa kote, pamoja na mapambo kufuatia habari hizo za kuvunja moyo.
Wageni waliohudhuria hafla hiyo na kushiriki video kwenye Tik Tok waliwashauri warembo kuwafanyia wapenzi wao ujasusi wa kutosha kabla ya kukubali kuolewa nao.
TAZAMA VIDEO
Social Plugin