Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BUNGE LA AFRIKA LATUMA SALAMU ZA POLE VIFO VYA WATU 250 KUFUATIA KIMBUNGA FREDDY NCHINI MALAWI NA MSUMBIJI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Afrika Kusini

Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) limetuma salamu za pole na rambirambi kufuatia vifo vya watu 250 katika nchi za Kusini Mwa Afrika (Malawi na Msumbiji) kutokana na Kimbunga Freddy kilichoambatana na upepo mkali na mvua kubwa.

Rais wa Bunge la Afrika (PAP) , Mhe Chifu Fortune Charumbira amesema Bunge la Afrika limehuzunishwa na tukio la Kimbunga Freddy baada ya kuzipiga nchi hizo za kusini mwa Afrika hivyo Bunge la Afrika linatoa pole kwa nchi za Malawi na Msumbiji.

Aidha, Chifu Charumbira amesema Bunge la Afrika lipo pamoja na Wamalawi na Wana Msumbiji wote katika kipindi hiki kigumu.

Rais huyo wa Bunge la Afrika pia ameshauri hatua madhubuti na maksudi zinapaswa kuchukuliwa ikiwa ni sehemu ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Akitoa taarifa kuhusu taarifa kuhusu madhara ya Kimbunga Freddy kilichoikumba ya Malawi na Msumbiji wakati wa Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16, 2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini, Mbunge kutoka Malawi Mhe. Steven Mikaya amesema idadi ya watu waliofariki kutokana na Kimbunga Freddy nchini Malawi na Msumbiji hadi sasa ni watu 250 na manusura ni wengi na huduma za kijamii zimekosekana barabara zimeharibiwa, hakuna huduma ya maji , umeme umekatika, uharibifu mkubwa umefanyika hivyo panahitajika misaada ya kibinadamu.

Amesema Malawi ndiyo nchi iliyoathirika zaidi na kimbuga Freddy, ambapo watu 250 wamepoteza maisha yao kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosomba nyumba kadhaa nchini humo.

Watu wengi na nyumba zao wamesombwa na matope katika mji mkuu Blantyre nchini Malawi ulioharibiwa zaidi baada ya kimbunga Freddy kupiga kusini mwa Afrika kwa mara ya pili, na kusababisha mafuriko ambayo yamewaua watu zaidi ya 250.

Vikosi vya uokozi vinaonya juu ya uwezekano wa kuwepo waathirika zaidi wa kimbunga hicho wakati vikiendelea kuwatafuta manusura kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na kimbunga Freddy.

Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Malawi Felix Washoni amesema waliwapata watu kwenye miti, kwenye mapaa ya nyumba au katika maeneo ya miinuko.

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera tayari ametangaza hali ya janga nchini Malawi.

Kimbunga hicho ambacho kinatajwa kuwa moja kati ya dhoruba kali zaidi kuwahi kurekodiwa, kilipiga maeneo ya Kusini mwa Afrika mwishoni mwa wiki hadi kuelekea siku ya Jumatatu wiki hii.

Kulingana na shirika la hali ya hewa duniani, Kimbunga Freddy kinaweza pia kuvunja rekodi ya kimbunga cha tropiki kilichodumu kwa muda mrefu zaidi. 

Kimbunga Freddy kwa mara ya kwanza kiliipiga Madagascar, Februari 21 na kuharibu eneo kubwa la kisiwa hicho kabla ya kufika Msumbiji Februari 24 na kusababisha vifo vya idadi kuwa ya watu kwenye mataifa hayo yote mawili na wengine kama 400,000 wakiwa wameathiriwa kwa namna moja ama nyingine.

Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ukiongozwa na Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Chief Fortune Charumbira unaendelea leo Machi 16, 2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ambapo wabunge wanajadili mambo mbalimbali kuhusu Bara la Afrika.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira akizungumzia tukio la Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji na kusababisha vifo vya watu 250
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira akizungumzia tukio la Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji na kusababisha vifo vya watu 250
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira na Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu 250 waliofariki kufuatia Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji.

Mbunge kutoka Malawi Mhe. Steven Mikaya akitoa taarifa kuhusu Kimbunga Freddy (Statement on the situation in Malawi in the Aftermath of Cyclone Freddy) kilichosababisha vifo vya watu 250.
Mbunge kutoka Malawi Mhe. Steven Mikaya akitoa taarifa kuhusu Kimbunga Freddy kilichosababisha vifo vya watu 250 nchini Malawi na Msumbiji
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ,Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 

 Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika ukiendelea leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya AfCFTA , Wamkele Mene, akihutubia Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP)

Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika ukiendelea leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Afrika Kusini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com