Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na Sheria imetembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga ambalo linaendelea kujengwa kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kimashtaka karibu na wananchi.
Akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo kwa kamati
hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul amesema kuwa Septemba 26
mwaka 2022 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliingia Mkataba na Mkandarasi Eliroi
Construction kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa
Shinyanga wenye thamani ya Bilioni 2.15 ikijumuisha ongezeko la Thamani VAT.
Gekul amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika
ndani ya muda wa miezi 8 ambapo ulianza kutekelezwa Novemba 22,2022 ambapo
unatarajia kukamilika June 22 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 35.
Gekul ameongeza kuwa mpaka sasa
mkandarasi amekwishalipwa fedha za awali kiasi cha shilingi milioni 323 kati
ya bilioni 2.15 huku Mkandarasi Mshauri Mwelekezi wa mradi Water Institute Kawazulite maombi ya kulipwa kiasi cha shilingi milioni 335.5
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester
Mwakitalu ameishukuru Kamati hiyo kwa juhudi zake kubwa za kuipigania Ofisi
hiyo ambapo kwa mwaka huu wa fedha unaondelea jumla ya mikoa sita imepatiwa
fedha za ujenzi wa Ofisi ikiwa ni pamoja na Shinyanga,Geita,Manyara, Rukwa,
Katavi na Njombe na kufanya idadi ya ofisi zinazojengwa kufikia kumi.
DPP Mwakitalu ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga
chini ya Mkuu wa Mkoa huo Christine Mndeme kwa kuwapatia eneo la Kiwanja kwa
ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo ambayo itasaidia na kurahisisha utoaji wa huduma
kwa jamii juu ya masuala ya Mashtaka ambapo amesema eneo hilo awali ilipewa
taasisi nyingine.
DPP Mwakitalu amesema kuwa ujenzi huo utakapokamilika
utarahisisha utaoaji wa huduma kwa jamii ambapo watumishi watakuwa na sehemu
bora na mazingira rafiki ya utaoji wa huduma kwa wananchi.
Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi huo kampuni
ya Eliroi Construction Bw Ngakuka Ngakuka amesema kuwa mradi huo umechelewa
kufikia asilimia 50 mpaka sasa kutokana na kuchelewa kwa malipo ya awali
sambamba hilo Ngakuka amesema kuwa licha ya kuraisi cheti cha malipo yanakwama
kutoka kwa wakati
Nao baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Boniphace
Butondo wamesema kuwa msukumo mdogo wa utoaji wa fedha unachangia kasi ndigo ya
ujenzi wa majengo hayo ambayo yanapaswa kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa
huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Christine Mndeme ameahidi
kamati hiyo kuwa atahakikisha anaisimamia kwa ukaribu ujenzi huo ili uweze
kukamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa ya utaoji wa huduma kwa
jamii.
Mndeme ameishukuru serikali kwa kutoa fedha hizo kwa
ajili ya ujenzi wa mradi huo kwani muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga
huku akiongeza kwa kuwa mradi huo unakwenda kubadili mandhari ya Mkoa wa
Shinyanga
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo amemtaka mkandarasi kuongeza kasi
ya ujenzi kwa kuwa muda aliyopewa mpaka sasa ni zaidi ya miezi minne mradi huo
bado uko asilimia 35 ambapo alipaswa kuwa asilimia zaidi ya 50.
Kyombo amesema kuwa lengo la ujenzi wa Ofisi hizo ni
kusogeza huduma karibu na wananchi hivyo usimamizi Madhubuti unapaswa kuwepo
ili kuondoa mikwamo ya ujenzi huo isiyo kuwa na tija katika ujenzi huo
Aidha Kyombo ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za
ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itakayosaidia utoaji wa huduma
bora kwa wananchi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na
Sheria leo imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali
inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Manispaa
ya Shinyanga.
Social Plugin