Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 24 ameaga dunia baada ya kujeruhiwa katika vita vya wanandoa wawili eneo la Rachuonyo Kasikazini katika kaunti ya Homa Bay nchini Kenya.
Dan Ouma anaripotiwa kujaribu kuwatenganisha wanandoa wawili waliokuwa wakipigana lakini badala yake akapigwa na kifaa kichwani butu katika vita hivyo.
Akithibitisha kisa hicho, Chifu wa kata ya Kanyaluo Magharibi Elius Ombim amesema kuwa mwanaume mmoja kutoka kijiji ca Seme Kaloo alikuwa akipigwa na mke wake na watoto kufuatia mzozo wa nyumbani.
Hili lilisababisha majirani - akiwemo Ouma - kuingilia kati lakini akawa ndiye aliyebeba msalaba wa vita hivyo.
Alipigwa kwa kifaa butu kichwani na kukimbizwa hadi Hospitali ya Kadienge kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay akiwa hali mahututi.
Kwa bahati mbaya, aliaga dunia katika hospitali hiuo akipokea matibabu na mwili wake kuhamishiwa katika makafani ya Homa Bay.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin