Shimo chumbani alimofukiwa marehemu
Mwanamke aitwaye Salma Maulid mkazi wa Mtaa wa Mbilani Kata ya Kidongo Chekundu Manispaa ya Tabora, ameuawa na mtu anayedaiwa kuwa ni mumewe kisha mwili wake kufukiwa chumbani, chini ya uvungu wa kitanda.
Tayari mwili wa marehemu umefukuliwa na Jeshi la Polisi limetangaza kumsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye alitoweka kusikojulikana baada ya kutekeleza tukio hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi.
Amesema mtuhumiwa baada yakutekeleza tukio hilo amekimbia.
Social Plugin