Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum akizungumza wakati wa Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
amekemea vikali makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka wanaCCM kumuunga Mkono Mbunge aliyepo madarakani Mhe. Patrobas Katambi huku akiwasisitiza WanaCCM kuacha kutengenezeane ajali na kwamba viongozi waliopo madarakani wasilinganishwe na walio nje ya madaraka.
Bandola ameyasema hayo leo Jumatano Machi 29,2023 wakati Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini ikiadhimisha Wiki ya Jumuiya hiyo sambamba na mafunzo ya uongozi wa Viongozi wa jumuiya hiyo waliochaguliwa mwaka 2022 ambapo alikuwa Mgeni rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga John Siagi.
Amewataka wanachama wa CCM na viongozi wa CCM kuepuka kugombanishana kwani kufanya hivyo kunayumbisha Chama hicho.
“Tusitengenezeane ajali, waliopo madarakani wasilinganishwe na walio nje ya madarakani, Mbunge wetu, madiwani wetu pia wasilinganishwe na viongozi wa serikali. Ukiona mwanachama analinganisha mbunge na mkurugenzi wa halmashauri hiyo siyo sawa, kila mmoja usimamiaji wake ndiyo maendeleo yanakuja, akiwa diwani bubu hawezi kuleta maendeleo. Diwani nenda kwa mkurugenzi mwambie kata yangu sioni maendeleo,yale maendeleo yakija mpeni sifa diwani, mbunge”, amesema Bandola.
“Acheni makundi, mtaliwa pesa zenu bure, muacheni mbunge afanye kazi, na msimlinganishe kiongozi aliyepo madarakani na watangulizi wake, wapeni ushirikiano”,amesema Bandola.
“Waliopo nje ya uongozi wasipambane na walio ndani ya uongozi na waliopo ndani ya uongozi wasipambane na wanachama waliopo nje ya uongozi, tusitengenezeane ajali…Haya ndiyo maadili tunayotaka”,ameongeza Bandola.

Salum Bandola
Pia amesisitiza Jumuiya kuwa na miradi hivyo kusisitiza kuwa na miradi na kuisimamia sambamba na kuongeza wanachama wapya kwani dhamira ya CCM ni kuongoza dola.
“Kuanzia shina, tawi , kata twendeni tukasake wanachama ili tusiwe na kazi ngumu katika kushika dola”,amesema Bandola.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Fue Mlindoko amekemea mambo ya ushoga akisisitiza kuwa suala la ushoga siyo suala la kulichezea hivyo kuwataka wazazi kuwakagua watoto wao kila siku kwani dunia imeharibika.
“Hili suala la ushoga siyo suala la kulichezea, limeleta upotoshaji mkubwa kwa familia zetu, kumbe kuna mkurugenzi wa Ushoga nchini?, kuna viongozi wa ushoga kwenye mikoa?!, hawa wamejipanga kuharibu taifa letu, kuharibu vijana wetu, kuharibu watoto wetu”,amesema Mrindoko.
“Ndugu zangu wazazi niwaombe tuzikague familia zetu kila siku, mtoto ametoka shule akija mkague, mkague kweli kweli kwa sababu dunia yetu imeharibika, siku hizi hata sisi akina babu eti na sisi tunawalawiti wajukuu zetu, tunalawiti, tutakuwa na taifa la jinsi gani, taifa la mashoga? Haiwezekani tuwe na taifa la mashoga, sisi wazazi ndiyo wa kusimama mbele kweli kweli kuzuia upuuzi huu unaotengenezwa na mataifa ya Magharibi yanayotuharibia taifa letu”,ameongeza Mlindoko.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Fue Mlindoko.
“Tuwakagueni watoto wetu, akitoka shule mvue suruali mkague, usiogope kuliko mtoto kuharibiwa, tukatae, tusikubali ushoga, sasa litakuwa taifa la mashoga, tuikataeni hii hali, na ishindwe kweli kweli na ndiyo maana tunaitwa wazazi”,amesisitiza Mlindoko.
Katika hatua nyingine amekemea tabia ya baadhi ya wanachama na viongozi wa Chama ambao wakitumwa kazi hawataki, wakipewa maagizo ya kufanya kazi wanapinga.
“Unakuta mtu anapinga viongozi waliochaguliwa, anapinga mbunge aliyepo madarakani wakati ni kiongozi halali. Tupendaneni ndugu zangu waacheni waliopo madarakani wafanye kazi, acheni makundi makundi, na tukikugundua unapinga viongozi na maagizo yanayotolewa tutakuchukulia hatua za kinidhamu”, amesema Mlindoko.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi amesema katika kujikwamua kiuchumi jumuiya hiyo inaendelea kupambana na kwa kushirikiana na viongozi na wadau ili kuhakikisha mambo yao yanaenda vizuri na hivi karibuni wataanzisha mradi wa kufyatua matofali.
Aidha amehimiza kila kiongozi wa CCM kuhamasisha wanachama kulipa ada, kufanya vikao mara kwa mara.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi amewataka WanaCCM kutatua migogoro inayotokea kwa baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa badala ya kuwakataa kwenye mikutano ya hadhara
"Suala la ku organize watu kukataa viongozi kwenye mikutano ya hadhara halikubaliki, hiyo ni sawa na kuikataa CCM. Ukitokea mgogoro unaomhusu mwenyekiti wa serikali ya mtaa jambo hilo lishughulikiwe ndani ya chama",amesema.
Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum akizungumza wakati wa Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023 katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum akizungumza wakati wa Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023 katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Fue Mlindoko
akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Fue Mlindoko akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023
akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023
Keki maalum wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023

Katibu wa Mbunge Shinyanga Mjini Samwel Jackson akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Samwel Jackson akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Katibu wa Vijana CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Faraji Katambalambula akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mwakilishi wa Vijana kwenda Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Peter Frank Alex akitoa mada ya Uongozi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Shinyanga mjini, Hasna Maige akitoa mada ya masuala ya ukatili wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini. Daniel Kapaya akitoa mada ya Malezi na Makuzi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Richard Mseti akitoa mada kuhusu Mazingira wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini Esha Stima akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Katibu wa CCM wilaya ya Bariadi Masanja Salu (aliyewahi kuwa katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga) kizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mwenyekiti wa Vijana CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Madete akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini

Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya Wiki ya Wazazi CCM na Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatano Machi 29,2023

Social Plugin