Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YAWE, RESTLESS WAENDESHA MDAHALO KUHUSU UTEKELEZAJI NA UFUATILIAJI WA LENGO 16.7.2 LA MAENDELEO ENDELEVU....VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA UONGOZI

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Youth And Women Emancipation (YAWE) kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika lisilo la Kiserikali la Youth And Women Emancipation (YAWE) kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development limeendesha Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania huku vijana wakihamasisha kuchangamkia fursa za uongozi na kushiriki katika ngazi za maamuzi.
Kupitia Mdahalo huo uliofanyika leo Ijumaa Machi 31,2023 Mashirika hayo yamewasilisha Matokeo ya utafiti wa vijana juu ya hali ya utekelezaji wa lengo namba 16.7.2 la malengo ya maendeleo endelevu Tanzania uliofanyika kupitia Mradi wa Kijana Wajibika unaotekelezwa na Shirika la YAWE kwa kushirikiana na Restless Development katika kata za Ndala na Masekelo katika Manispaa ya Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Restless Development kupitia Shirika la Ford Foundation.

Akifungua Mdahalo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amewataka vijana kuwa Viherehere wa maendeleo na kuhakikisha wanachangamkia nafasi za uongozi kuanzia serikali za mitaa na mikopo inayotolewa na halmashauri ya wilaya.

“Serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa vijana, ichangamkieni, njooni kwenye halmashauri mpate mikopo lakini pia changamkieni fursa zinazotolewa kwenye mashirika na wadau mbalimbali…Kijana unatakiwa kuwa na kiherehere cha maendeleo”,amesema Tesha.

“Jitokezeni kugombea nafasi za uongozi kuanzia kwenye serikali za mitaa na nafasi zingine za uongozi,vijana mnaweza”,ameongeza Tesha.

Kwa upande wake, Afisa Miradi wa Shirika la Restless Development, Damian Luteli amesema Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu umebebwa na Matokeo ya utafiti wa vijana kutoka mikoa 18 uliofanyika mwaka 2021/2022 ambapo matokeo yake yanasisitiza uhitaji wa vijana kushiriki katika masuala ya uongozi na ngazi za maamuzi lakini pia vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali na wadau ili kujikwamua kiuchumi.

Naye Afisa Miradi wa Shirika la YAWE, Moshi Jilalage amesema mradi wa Kijana Wajibika unataka vijana kujitambua na kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali ili kujikwamua lakini pia vijana kushiriki katika ngazi za maamuzi/kuwania uongozi.

Jilalage ametumia fursa hiyo kuiomba serikali na wadau kuendelea kuwashika mkono vijana na kuwashirikisha katika ngazi za maamuzi.

Afisa Vijana wa Shirika la YAWE, Method Stephen amesema Shirika la YAWE na Restless Development wameendesha mdahalo huo kwa lengo la kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa vijana kwenye ngazi za maamuzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kijana Wajibika unaolenga kuhakikisha kuna ushiriki na ushirikishwaji wa vijana hususani wa kike na watu wenye ulemavu kwenye ngazi za maamuzi.

“YAWE inatekeleza mradi wa Kijana Wajibika katika wilaya ya Shinyanga katika kata za Ndala na Masekelo. Leo tumekutana na vijana kutoka kata ya Ndala, Masekelo, Ngokolo na Ndembezi na kuendesha Majadiliano baina ya vijana, viongozi na wadau yakiongozwa na mada Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu na tumewasilisha Matokeo ya utafiti wa vijana juu ya hali ya utekelezaji wa lengo namba 16.7.2 la malengo ya maendeleo endelevu Tanzania”,amesema Stephen.

Nao vijana walioshiriki Mdahalo huo wamesema kupitia mdahalo huo wamejengewa uwezo na kupewa ujasiri wa kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali na wadau ili kujikwamua kiuchumi na kuahidi kuwajibika na kuchukua hatua za kuwania uongozi na kushiriki katika ngazi za maamuzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Youth And Women Emancipation (YAWE) kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Youth And Women Emancipation (YAWE) kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Youth And Women Emancipation (YAWE) kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Youth And Women Emancipation (YAWE) kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development.
Afisa Miradi wa Shirika la YAWE, Moshi Jilalage akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania

Afisa Miradi wa Shirika la Restless Development, Damian Luteli akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania 

Afisa Vijana wa Shirika la YAWE, Method Stephen akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania
Afisa Maendeleo Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania
Afisa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Manispaa ya Shinyanga, Bestina Gunje akizungumza wakati wa Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu Tanzania
Mdahalo kuhusu Utekelezaji na ufuatiliaji wa lengo 16.7.2 la maendeleo endelevu ukiendelea

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com