Baadhi ya matukio Kwa njia ya picha yaliyofanyika kwenye Mkutano wa Taasisi ya ABAROLI na wadau wa maendeleo.
Na Dotto Kwilasa, DODOMA.
TAASISI ya ABAROLI (American Bar Association Rule of Law Initiative) imetoa elimu kuhusu umuhimu wa kujieleza (Freedom of Expression) kwa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchochea maendeleo ya know wa tansia ya habari nchini.
Akifungua warsha hiyo jijini Dodoma,Hakimu Mkazi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (Dodoma)Florah Mhelela amesema ibara ya 18 ya Katiba inatoa haki ya Uhuru wa kujieleza hivyo ni vyema kufanyiwa kazi kama inavyoelekezwa.
“Bila kuathiri sharia ya nchi Kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,kutafuta habari…na ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.Hivyo ni lazima twende moja kwa moja kujua sheria inasema nini na Katiba inavyotaka.” Amesema.
Kutokana na hayo,Mwakilishi wa kundi hilo la Wabunge, Mheshimiwa Nusrat Hanje amepongeza hatua ya taasisi hiyo kuendelea kupambania ustawi wa tasnia ya habari na kueleza kuwa itawawezesha wabunge kuwa katika nafasi nzuri ya kujadili masuala yanayohusu uhuru wa kujieleza.
Hata hivyo Mbunge huyo ameshauri taasisi hiyo kuongeza wigo ili waweze kuwafikia wabunge wengi zaidi na kwamba itasaidia kukuza uhuru wa vyombo vya habari nchini Kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa meneja wa mradi huo Violah Ajok amesema ABAROLI imeendelea kutoa elimu hiyo kundi la wabunge kutoka nchi za Afrika Mashariki ili kuboresha sheria zinazosimamia haki hiyo hususani katika tasnia ya habari.
Social Plugin