





Picha ya pamoja ya wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) akizungumza katika uzinduzi wa Baraza la Pili la TEA.
************************
Baraza la Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) limenzinduliwa ramsi tarehe 24 Machi, 2023 mjini Singida ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya kuwashirikisha wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahala pa kazi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini pamoja na sheria ya Utumishi wa Umma.
Baraza hilo limezinduliwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Michael John ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Bw. John amesema mabaraza ya Wafanyakazi mahala pa kazi yanaundwa na kulindwa na Sheria kutokana na Serikali kutambua umuhimu wa kushirikisha watumishi katika maamuzi na mipango ya maendeleo ya Taasisi na maslahi ya watumishi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi Bahati Geuzye amewakumbusha wajumbe wa Baraza kuwa, wanajukumu muhimu la kuchangia ufanisi wa utendaji wa Mamlaka kupitia majadiliano na ushauri wao kama wajumbe wa chombo hiki muhimu.
“Ili Taasisi ifikie Malengo yake ni lazima kuwepo na ushirikiano wa dhati kati ya Bodi na Menejimenti, Menejimenti na watumishi lakini pia kati ya watumishi wenyewe kwa wenyewe” Amesema Bi. Geuzye
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya Umma inayofanya kazi chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
TEA inaratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao unasaidia jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa.
Pia TEA inaratibu Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia
Social Plugin