SHIRIKA LA WEADO LIMEANZA KUTEKELEZA MRADI WA KAMPENI YA CHANJO YA UVIKO-19 WILAYANI SHINYANGA


Shirika la WEADO likiendesha Kampeni ya utoaji Chanjo ya UVIKO-19 wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Women Elderly Advocacy And Development Organization (WEADO) limeanza kutekeleza mradi wa Kampeni ya Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi wilayani Shinyanga, hasa Makundi ya Wazee, Vijana na Wanawake, ili wajitokeze kupata Chanjo hiyo na kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Corona pale watakapoambukizwa na wasipate madhara makubwa.

Ofisa miradi kitoka Shirika la WEADO Winnie Hinaya, akizungumza jana wakati alipokutana na Mabalozi wa kuhamasisha Chanjo hiyo kutoka Makundi ya Wazee, Vijana na Wanawake katika Kata ya Tinde na Didia wilayani Shinyanga, amesema mradi huo ni wa miezi mitatu ambao unafadhiliwa na UNICEF kupitia mdau kiongozi Help Age Tanzania.

Amesema mradi huo ni wa majaribio ambao watautekeleza katika Kata Sita za wilayani Shinyanga ambazo ni Tinde, Didia, Masengwa, Usanda, Iselamagazi, Solwa na utakwenda sambamba na kupinga vitendo vya utakatili wa kijinsia, pamoja na uinuaji wananchi kiuchumi ikiwamo na kuchangamkia mikopo ya Halmashauri asilimia 10.

“Lengo la mradi huu ambao ni wa majaribio ni kuhamasisha jamii ijitokeze kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19 ili siku wakipata maambukizi wasipate madhara makubwa na kuendelea kuwa salama,”amesema Hinaya.

Naye Helena Maleza akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la WEADO, amesema katika Kampeni hiyo kutukuwa na utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupata Chanjo, pamoja na kuondoa imani potofu ambayo imejengwa kwa wananchi kuwa Chanjo hizo zina madhara, na kutakuwa na ushuhuda mbalimbali kwa wananchi ambao wamepata Chanjo na hawakupata madhara yoyote.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Anderson Lyimo, amewataka wananchi hasa wazee kupuuza upotoshaji juu ya Chanjo ya UVIKO-19, na kuwasihi wawe mstari wa mbele kujitokeza kupata Chanjo hiyo, ili siku wakipata maambukizi wasipate madhara makubwa na kuokoa maisha yao.

Lyimo ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wazee Taifa, amesema wazee kinga zao zimeshashuka tofauti na vijana, hivyo wakipata maambukizi ya Corona wanakuwa katika hatari zaidi ya kupoteza maisha, lakini wakipata Chanjo hawatapata madhara makubwa. 
 
“Mimi nimepata Chanjo ya UVIKO-19 tangu Agost mwaka 2021 na sijapata madhara yoyote hadi sasa na afya yangu ni imara, na baadhi ya magonjwa madogo ambayo yalikuwa yakinisumbua mfano mafua na vikohozi hayapo tena, hivyo nawasihi wazee wenzangu hasa wa vijijini jitokezeni mpate Chanjo ni salama na haina madhara yoyote puuzeni imani potofu,”amesema Lyimo.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Kata ya Didia wilayani Shinyanga Engelbert Kidutu, amesema awali hakuwa tayari kupata Chanjo lakini baada ya kupewa elimu vizuri na kuondolewa imani Potofu, jana ameamua kupata Chanjo hiyo, na kuomba wataalamu wa afya waendelee kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili wachanjwe.

Helena Malesa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la (WEADO) kwenye kikao cha Mabalozi wa kuhamasisha kampeni ya Chanjo ya UVIKO-19 Makundi ya Wazee, Vijana na Wanawake Kata ya Tinde wilayani Shinyanga, pamoja na kuinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ofisa Miradi kutoka Shirika la (WEADO) Winnie Hinaya akizungumza kwenye kikao hicho.

Ofisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka Shirika la WEADO John Eddy, akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu wa Baraza la Wazee mkoani wa Shinyanga na Taifa Anderson Lyimo akizungumza kwenye kikao hicho.

Wajumbe wa Baraza la Wazee Kata ya Tinde wilayani Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Ofisa Miradi kutoka Shirika la WEADO Winnie Hinaya (kushoto) akiwa na Mtendaji wa Kata ya Didia wilayani Shinyanga Monica Mpolosi kwenye kikao cha Mabalozi wa kuhamasisha Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kutoka Makundi ya Vijana, Wazee na Wanawake.

Wajumbe wa Baraza la Wazee Kata ya Didia wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Ofisa Tathimini na ufuataliaji kutoka Shirika la WEADO John Eddy akiwa kwenye kikao hicho.

Katibu wa Baraza la Wazee Kata ya Didia wilayani Shinyanga Engelbert Kidutu (kulia) akipata Chanjo ya UVIKO-19 mara baada ya kupewa elimu kuwa Chanjo hiyo ni salama.

Ofisa Afya Kata ya Didia wilayani Shinyanga Edwardina Maganga akiendelea kutoa Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi ambao wamehamasika mara baada ya kupewa elimu Chanjo hiyo ni salama.


Ofisa Afya Kata ya Didia wilayani Shinyanga Edwardina Maganga akiendelea kutoa Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi ambao wamehamasika mara baada ya kupewa elimu Chanjo hiyo ni salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post