Kajala Jeremia Katibu Mwenezi na itikadi kata ya Imesela akizungumza kwenye ziara ya kamati ya Chama Cha mapinduzi.
OFisi ya serikali ya kijiji chaMwamanyuda kata ya Imesela iliyojengwa na sungusungu,nguvu za wananchi na mfuko wa serikali.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyika akitoa taarifa mbele ya kamati ya chama.
Diwani wa kata ya Imesela Seth Msangwa akizungumza katika mwendelezo wa ziara ya siasa ya kamati ya chama cha Mapinduzi.
Na Halima Khoya,Shinyanga.
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Imesela halmashauri ya Shinyanga imeutaka uongozi wa shule ya Msingi Nyika kufanya kikao na uongozi wa serikali ya kijiji ili kuitisha mkutano wa hadhara na wananchi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo cha walimu pamoja na wanafunzi.
Maagizo hayo yametolewa Machi 10,2023 kwenye mwendelezo wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Imesela baada ya kutembelea mradi unaoendelea katika shule hiyo na kukuta ujenzi wa umesimama.
Diwani wa Kata ya Imesela Seth Msangwa amesema ujenzi wa choo cha walimu umetumia muda mrefu kukamilika kutokana na changamoto tofauti ikiwa ni pamoja na ushirikiano mdogo wa wananchi na uongozi wa kijiji ambapo amewataka kuitisha kikao kwa ajili ya kuchangia ujenzi huo ili kuweka mazingira salama kwa walimu na wanafunzi.
Msangwa amesema katika ujenzi wa choo cha walimu atachangia saruji, kuleta mtu wa kufyatua matofali na mchanga na kwamba miongoni mwa changamoto walizozikuta watazichukua na kuzipeleka kwenye uongozi wa juu huku changamoto zingine amewataka wananchi na uongozi wa kijiji kukaa kikao kujadili uwiano uliopo kati ya vyoo vya wanafunzi na idadi ya wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo ambavyo havina kiwango.
"Kipindi naomba nafasi katika eneo hili niliahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wote lakini kama nyie msipokuwa na ushirikiano tutafikiaje malengo, Kaeni chini muijenge Nyika yenu, hali ya vyoo vya wanafunzi ni mbaya na wala sitaki kupaona,kaeni na wananchi mchangie ili hata serikali iwe na wepesi kutia mkono wake baada ya nyie kuanza",amesema Msangwa.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Imesela,Richald Nyanda amesema katika shule hiyo kuna uhaba wa matundu ya vyoo kutokana naa idadi ya wanafunzi iliyopo na kwamba hali iliyopo kwenye matundu hayo ni mbaya hali inayohatarisha afya kwa waafunzi.
"Taarifa uliyotupa na uhalisia uliopo Nyika hatuna vyoo hata wewe ukienda saivi unaweza ukaogopa kuingia, watoto wetu wana hali mbaya, kufikia tarehe 25 kuwe na kamati mpya ya kijiji, matundu yanayohitajika ni 21 na yaliyopo ni 6 alafu tumekaaa tu hakuna utaratibu wa kujenga mengine,bada ya kikao hicho itisha serikali ya kijiji ili kushughulika na hili",amesema Nyanda.
Awali akitoa taarifa ya shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyika,Marco Sylivester amesema kuwa Shule hiyo ina matundu ya vyoo 6 na uhitaji wa matundu ya vyoo 21 pia ina uhaba wa matundu ya vyoo vya walimu mawili na kwamba inafanya taratibu za kujenga vyoo hivyo ambavyo vimefikia kwenye msingi.
"Shule ya Msingi Nyika ina wanafunzi 512 na walimu 8, shule ina madarasa 8 mahitaji 21,mahitaji ya matundu ya vyoo vya walimu ni 02 yaliyopo ni 0, shule ina jumla ya wanafunzi 83 kwa miaka miwili waliofanya mtihani ni 82 waliofaulu 46,waliofeli 37 ambayo ni sawa na asilimia 57%,Tutafanyia kazi maagizo yote tuliyopewa",amesema Sylivester.