NSSF SHINYANGA YAENDESHA SEMINA KWA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI KATIBU TAWALA PROF SIZA AWATAKA WAAJIRI WASIKWEPE KUPELEKA MICHANGO YA WATUMISHI WAO NSSF

NSSF Shinyanga wakitoa Semina kwa Waajiri wa Sekta Binafsi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga imeendesha Semina ya waajiri katika Sekta Binafsi, ili kuwa kumbusha majukumu yao na wajibu katika kuwahudumia watumishi wao ikiwamo kuwaunga na NSSF na kuwawekea akiba ya mafao kwa kupeleka michango.

Semina hiyo imefanyika leo Machi 18, 2023 katika ukumbi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kudhuliwa na Waajiri wa Sekta Binafsi, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof, Siza Tumbo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo Katibu Tawala Prof Siza, amewataka Waaajiri wa Sekta Binafsi kuhakikisha wanawaunga watumishi wao na Mifuko ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii pamoja na kuwasilisha michango yao ili kuwaekea akiba ya uzeeni pale watakapo Staafu kufanya kazi, ili wawe na fedha ambazo zinatwasaidia katika maisha yao.

“Sekta Binafsi katika nchi yetu ya Tanzania ndiyo inatoa ajira kubwa kuliko Serikali, hivyo watumishi wao wasipo kuwa na akiba kwenye mifuko ya kifadhi ya jamii hapo baadae watakapo staafu tutakuja kuwa na taifa la omba omba,”amesema Prof. Siza.

“Nawapongeza pia NSSF kwa kutoa elimu kwa Wakulima, Bodaboda, Bajaji ili wajiunge na mfuko huu na kujiwekea akiba ya baadae na kuishi maisha mazuri sababu watakuwa na fedha za kujikimu kimaisha watakapokuwa hawana nguvu tena ya kufanya kazi,” ameongeza Prof. Siza.

Katika hatua nyingine amewataka watumishi pale ajira zao zitakapokoma kabla ya kustaafu wasiende kuchukua fedha za akiba zao NSSF, sababu fedha hizo lengo lake ni kuwasaidia pale watakapo staafu kufanya kazi kwa kufikisha umri wa miaka 60.

Naye Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi, amewasihi Waajiri wawe wanalipa michango kwa wakati NSSF ili kuwawezesha kulipa mafao kwa wakati, na vilevile Waajiri  watumie mfumo wa Employer Portal kulipa michango.
Mfumo ambao ni rahisi unaomfanya Mwajiri kutekeleza majukumu ya kisheria ya NSSF popote alipo.

Aidha, amesema malengo ya Semina hiyo ni kuwakumbusha majukumu na wajibu wao Waajiri wa Sekta Binafsi katika kuwahudumia watumishi wao kuwaunga na NSSF pamoja na kupeleka michango ya akiba.

Nao Baadhi ya Waajiri wa Sekta Binafsi wamesema watatekeleza maelekezo ambayo yametolewa na Serikali kupitia kwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo, na kuahidi kuwaunga watumishi wao na NSSF pamoja na kupeleka michango ya akiba kwa wakati fedha ambazo zitawasaidia katika maisha yao ya kustaafu.

katika Semina hiyo zimewasilishwa mada mbalimbali ikiwamo ya kazi na majukumu ya NSSF kwa mujibu wa sheria, wajibu wa Waajiri kwa mujibu wa Sheria ya NSSF, Mafao ya NSSF na Taratibu zake, Employer Portal kulipa michango kwa NSSF kwa njia ya mtandao.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo akizungumza kwenye Semina ya Waajiri wa Sekta Binafsi iliyoandaliwa na NSSF.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akizungumza kwenye Semina hiyo.
Meneja wa NSSF Kahama Aisha Nyemba akizungumza kwenye Semina hiyo.
Afisa Matekelezo Mwandamizi kutoka NSSF Makao Makuu Bwayi Mlanga akiwasilisha Mada ya kazi na majukumu ya NSSF kwa mujibu wa sheria kwa washiriki wa Semina hiyo.
Afisa sheria Mwandamizi Karimu Kambagha, akiwasilisha mada ya wajibu wa Waajiri kwa mujibu wa sheria ya NSSF kwa washiriki wa Semina hiyo.
Afisa Mafao Ramadhani Salumu akiwasilisha mada ya Mafao ya NSSF na taratibu zake kwa washiriki wa Semina hiyo.

Afisa TEHAMA Mbwana Seleman akiwasilisha mada ya Employer Portal kwa washiriki wa Semina hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof, Siza Tumbo (katikati) akiwa na Meneja wa NSSF Shinyanga Amina Mdabi (kushoto) na Meneja wa NSSF Kahama Aisha Nyemba wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwa washiriki kwenye Semina hiyo.
Meneja wa NSSF Shinyanga Amina Mdabi (kulia) akiwa na Meneja wa NSSF Kahama Aisha Nyemba (kushoto) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwa washiriki kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semima hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semima hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semima hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semima hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Semina ya NSSF ikiendelea kwa Waajiri wa Sekta Binafsi.

Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Semina ya NSSF ikiendelea kwa Waajiri wa Sekta Binafsi.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kwenye Semina hiyo.
Semina ya NSSF ikiendelea kwa Waajiri wa Sekta Binafsi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post