Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : SHINYANGA WAFANYA KONGAMANO LA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA....WAJIVUNIA MAFANIKIO LUKUKI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kongamano hilo la Miaka Miwili ya Rais Samia likiongozwa na Kauli mbiu ‘Umethubutu, Unaweza, Kazi Iendelee’ limefanyika leo Jumamosi Machi 25, 2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi, vyama vya siasa na wananchi wa mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lililofanyika leo Jumamosi Machi 25, 2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde

Habari na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga umefanya Kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 25, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiwamo na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akielezea mafanikio ya Mkoa huo wa Shinyanga ndani ya miaka miwili ya Rais Samia, amesema zimeletwa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Akielezea mafanikio katika Sekta ya Afya, amesema Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 32.6 na kujengwa vituo mbalimbali vya Afya na Zahanati, pamoja na Sh.bilioni 7.8 kujengwa Hospitali ya Rufaa mkoani humo, na kuondoa adha ya wananchi kufuata huduma za matibabu Bugando Jijini Mwanza na Mhimbili.

Amesema pia Rais Samia katika Mkoa huo ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 14.9 na kununua Vifaa Tiba pamoja na Madawa na katika Mkoa huo kuna upatikanaji wa Madawa asilimia 89.

Akizungumzia Sekta ya Elimu ,amesema Rais Samia ametoa fedha Sh.bilioni 37.6 na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwamo ujenzi wa matundu ya vyoo, madawati, vyumba vya Madarasa, huku akitoa fedha zingine na kujengwa Chuo cha VETA wilayani Kishapu, pamoja na Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wa Sekta ya Maji, amesema Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 52.2 na kutekelezwa Miradi ya Maji 45, na katika mwaka wa fedha (2021/2022) RUWASA ilipokea Bilioni 29.5 na kutekelezwa miradi ya maji 29, pia kuna ujenzi wa miradi mipya ya maji 15 yenye thamani ya Sh.bilioni 24.3.

Amesema pia katika mwaka wa fedha (2022/2023) RUWASA Mkoa walipokea fedha Sh.bilioni 22.7 na kutekelezwa miradi ya maji 15 na kuondoa adha ya wananchi kutumia maji yasiyofaa.

Ameelezea mafanikio ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara, amesema katika utawala wake Rais Samia ndani ya miaka miwili, zimejengwa barabara nyingi ikiwamo ujenzi wa Makaravati, Madaraja pamoja na uwekaji wa Taa za Barabarani.

“Mkoa wa Shinyanga ndani ya miaka miwili ya utawala wa Rais Samia tunajivunia mafaniko makubwa ya kimaendeleo pamoja na mapinduzi ya kiuchumi, ikiwamo na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),”amesema Mndeme.

“Rais Samia ametoa tena fedha Sh.bilioni 21 kwa ajili walengwa wa mpango wa kunusuru Kaya maskini TASAF, huku zikitolewa Lesseni za uchimbaji madini 827 na Lesseni za wachimbaji wadogo 267,”ameongeza Mndeme.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia).

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amempongeza Rais Samia kwa kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo, na wameona mvua kubwa ya maendeleo na wataendelea kumuombea afya njema ili aendelee kuwatumikia vyema watanzania.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwa niaba ya Wabunge wote wa Mkoa huo, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi katika Mkoa huo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lililofanyika leo Jumamosi Machi 25, 2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lililofanyika leo Jumamosi Machi 25, 2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.  Mboni Mhita (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa ( wa pili kushoto), Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakicheza muziki wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lililofanyika leo Jumamosi Machi 25, 2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.  Mboni Mhita akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi, Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava.
Kwaya ya Walimu Manispaa ya Shinyanga ikitoa burudani wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mshereheshaji (MC) Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike akizungumza wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Burudani ya ngoma ikiendelea wakati wa Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan likiendelea

Kongamano la Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan likiendelea.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com