Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATARAJIO YA NCHI NIKUWA NA SHERIA BORA NA NZURI YA HABARI - WAZIRI NAPE


Waziri wa Habari, Mawasiliono na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza alipokuwa akifungua mkutano wa 12 wa Jukwaa la wahariri Tanzania TEF ulioanza leo Machi 29,2023 Mjini Morogoro.

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi katika mkutano huo wa siku nne ulioanza leo machi 29,2023 Morogoro.

Makamu Mwenyekiti TEF Bakari Machumu akitoa salamu za utangulizi na kutoa utambulisho kwa wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye Mkutano huo.

Waziri wa Habari, Mawasiliono na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile (kushoto) kwa niaba ya wahariri.

Waziri wa Habari, Mawasiliono na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifurahia jambo pamoja na Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile (kushoto) mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti huyo.

(PICHA NA HUGHES DUGILO)

MOROGORO

Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliono na Teknolojia ya habari imesema matarajio ya nchi nikuwa na sheria bora na nzuri za habari zitakazodumu kwa muda mrefu zaidi na sio sheria kandamizi zinazotiliwa shaka na wadau wa habari.

Akifungua mkutano wa 12 wa Jukwaa la wahariri Tanzania TEF Waziri wa habari, Mawasiliono na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha sekta ya habari ni pamoja na kuzipitia sheria zinazolalamikiwa na wadau ikiwemo sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016.

"kumekuwa na mabadiliko makubwa katika utendaji wa vyombo vya habari, ninawahakikishia wahariri marekebisho ya sheria ya Huduma ya habari ya mwaka 2016 tayari yapo Bungeni, nawasihi muwe na subira" amesema Nape.

Amesema serikali ya awamu ya sita inatambua na kuheshimu mchango wa sekta ya habari katika kuimarisha uchumi na utawala bora hivyo ni vyema kuwa na sheria zenye kuleta usawa na haki ya upatikanaji wa habari.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodautus Balile amesema kumekuwa na ushirikiano mkubwa kati ya Jukwaa la wahariri, wadau wa habari pamoja na waandishi wa habari jambo lililochangia kupungua kwa kesi nyingi mahakamani zinazohusisha vyombo vya habari na wanahabari hapa nchini.

"Katika kipindi kifupi kuna kesi nyingi za vyombo vya habari zinazofikishwa mahakamani zimepungua, hii ni kutokana na jukwaa hili kuwa karibu zaidi na vyombo vya habari katika kuelekeza namna ya kufuata maandili ya uandishi wa habari" amesema Balile

Mkutano wa 12 wa TEF ni mkutano wa kikatiba ambao kila mwaka wananchama wake hukutana kwa lengo la kukumbushana maswala mbalimbali ya taaluma ya habari ambapo kwa mwaka huu mkutanao huo umefanyika mkoani morogoroukiwa na kaulimbiu ya "Sheria ya Habari na Maendeleo ya Vyombo vya habari"

(PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI WA MKUTANO HUO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com